Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3. Kupumzika

Mwili huu ni lazima upumzike ili upate kujitengeneza upya wenyewe. Yatupasa kuwa na muda wa burudani na wa kupumzika ili kupunguza msongo utokanao na kazi pamoja na majukumu ya kifamilia. Bila kuwa na muda wa kutosha kupumzika mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi, mfadhaiko na hasira kali. Msongo huo wa moyo unaweza kuleta ugonjwa ambao utatulazimisha kuchukua pumziko letu ambalo miili yetu ilikuwa inataka kwa muda wote. Hakuna kitu cha badala cha kuweka mahali pa usingizi mzuri wa usiku.
 
Kuzichaji upya betri zetu za kiroho kwa kuweka utaratibu wa kila siku ni muhimu pia kwa afya yetu ya kimwili. Muda wa kila siku anaotumia Mkristo katika kutafakari, kusoma Biblia, na maombi utaweza kuuponya mwili pamoja na roho. Tunakuhitaji pia kupata pumziko ili kuuvunja mzunguko wa kazi, yaani, kuwa na siku ya kupumzika kila juma, na likizo ya mwaka au nusu mwaka.
 
Mazoezi Ya Mwili

Mazoezi ya mwili ni ya muhimu sana kwa afya yetu:
1. Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebisha shinikizo la damu.
2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto.
 
Mazoezi Ya Mwili

Mazoezi ya mwili ni ya muhimu sana kwa afya yetu:
1. Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebisha shinikizo la damu.
2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto.
 
Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yote mawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwa kawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi na msongo (stress).
 
Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva. Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wa kinga mwilini (immune system). Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi zaidi.
5. Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili.
 
Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo
7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.
 
Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo
7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.
 
Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili. Laweza kuwa ni jambo la busara kumwona mganga wako kabla ya kuanza mazoezi hayo. Lengo lako na liwe kujishughulisha na kila aina ya mazoezi hayo ya mwili ambayo yanaweza kulinganishwa na kutembea maili moja kwa dakika kumi na tano mara nne au zaidi kw ajuma.
 
5. Maji

Kwa vile maji ni ya lazima kwa kila seli mwilini, basi, ingetupasa kunywa maji mengi.
1. Kwa uzito, mwili wetu karibu asilimia sabini ni maji…
2. Mwili wetu unahitaji takribani visaga (quarts) viwili na nusu vya maji kila siku ili uweze kufanya kazi zake zote. Baadhi ya kazi hizo ni pamoja na mzunguko wa damu mwilini, kuondoa uchafu mwilini, kusafirisha virutubisho vya chakula mwilini, na kukiyeyusha chakula mwilini
3. Mtu wa kawaida anazo seli za ubongo kati ya billioni 15 na 40 hivi. Kila moja ya hizo ina maji asilimia 70 hadi 85. Maji ya kutosha kuweza kuzigawa seli hizo hukufanya uwe na akili iliyochangamka, halafu husaidia kuzuia mfadhaiko (depression) na hasira kali.
 
Si maji yale tu unayokunywa ambayo ni ya muhimu. Kuoga maji ya baridi kidogo au vuguvuvugu kila siku au kwa kutumia bafu ya manyunyu (shower) huboresha mzunguko wa damu mwilini, hivyo kuupa mwili na ubongo wako nguvu. Bafu ya manyunyu au kuoga kwa njia ya kawaida huweza pia kutuliza mishipa ya fahamu iliyochachamaa, ambayo inaweza kuleta ugonjwa kwa kudhoofisha mfumo wa kinga mwilini. Kuoga pia kunaondoa uchafu kutoka juu ya ngozi, pia kunaweza kupunguzahoma.
 
Nyama ya wanyama ina mafuta ya majimaji (saturated fat) na mafuta mazito kolestero [cholesterol], ambayo yote huongeza hatari ya kupatwa na shinikizo la damu, kupooza (stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usio wa kawaida, kisukari na magonjwa mengineyo. Leo matabibu wengi wanawashauri wale wanaokula nyama kula mnofu ule tu usiokuwa na mafuta, uliopikwa vizuri, pamoja na kula samaki na kufanya hivyo kwa nadra sana.
 
Kwa vile watu wanaokula chakula cha mimea wana afya bora zaidi, tena wanaishi kwa muda mrefu zaidi, wataalamu wengi wa lishe na afya wanatusihi sana sisi ili tupate kufikiria kukirudia chakula kile cha awali walichopewa wanadamu cha kokwa, nafaka na matunda pamoja na mboga za majani zilizoongezwa.
 
Ukitaka kuanza kula vyakula vya mimea, hakikisha kwamba unaelewa kwanza namna ya kuandaa lishe bora bila kutumia nyama. Ule kiasi cha chakula kinachomtosha mtu kula kwa siku (migawo [serving] mitano au sita hivi) ya aina mbalimbali za matunda, pamoja na kokwa [karanga n.k.] nafaka, maharage, kunde, mbaazi na mboga za majani. Mboga za majani za kijani na za njano, pamoja na machungwa ni za muhimu sana. Tumia unga wa nafaka isiyokobolewa na mchele mwekundu (brown rice) badala ya ule mweupe. Ulaji wako wa wanga na sukari za mchanganyiko ungekuwa katika migawo (servings) sita au zaidi kwa siku moja. Badilisha matumizi yako ya mafuta ya wanyama (samli, siagi, mafuta ya nguruwe, shahamu izungukayo figo, n.k.) kwa kutumia mafuta ya mimea. Lishe hiyo juu inatosha bila kutumia nyama kama wewe unatumia vitu vinavyotokana na maziwa.
 
Alkoholi huathiri mifumo ya mwili ifuatayo:
1. Mfumo wa kinga mwilini - Alkoholi inapunguza uwezo wa chembechembe nyeupe wa kupigana na ugonjwa, hivyo kuzidisha hatari ya kupatwa na nimonia (pneumonia), kifua kikuu, homa ya manjano, na kansa za aina kadhaa.
2. Mfumo wa tezi (endocrinesystem) zinazotoa majimaji mwilini - Vinywaji viwili tu au vitatu kwa siku huzidisha hatari ya kuharibika mimba, kuzaa watoto waliokufa, na watoto waliozaliwa kabla ya wakati wake.
3. Mfumo wa mzunguko wa damu mwilini Matumizi ya alkoholi huzidisha hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo, hupunguza sukari katika damu, na kuzidisha kiwango cha mafuta katika damu na kuongeza mapigo ya moyo, hivyo kuzidisha shinikizo la damu.
4. Mfumo wa kuyeyusha chakula - Alkoholi inaleta kuwasha tumboni, na kwa njia hiyo kusababisha kutoka damu katika tumbo hilo… Mazoea ya kutumia alkoholi huzidisha hatari kwa ini kuw ana mafuta mengi, homa ya manjano, na ugonjwa wa ini (cirrhosis).
 
Alkoholi inahusika na asilimia kubwa ya watu wanaojiua wenyewe, vifo vinavyosababishwa na magari, kuwatendea vibaya watoto, na ukatili uliomo nyumbani.

8. Kuutumainia Uweza Wa Mungu

Mtu anayesumbuliwa mara kwa mara na hofu au hatia ataona vigumu kwake kupata manufaa kamili kutokana na mazoea hayo ya afya tuliyotoka kuyaeleza muda mfupi tu uliopita. Lakini mtu yule mwenye imani isiyo na shaka kwa Mungu atapata chimbuko hili la mwisho litakalomletea hali njema katika maisha yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…