Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Changamoto

Jenipher anasema kazi hii ni ngumu na kama mtu hana moyo wa uvumilivu hataweza kuifanya kutokana na kudharaulika na baadhi ya abiria.

“Kuna baadhi ya abiria wana maneno ya karaha na maudhi kiasi kwamba kama una hasira unaweza kujikuta unagombana nao kila siku”, anasema Jenipher.
 
Inafika kipindi hata mtoto wangu humuuliza mama yake mdogo kuwa mbona simuoni mama, lakini ndio hivyo nitafanyaje nikisema nikae nyumbani tutashinda njaa”, anasema Jenipher

Anasema baada ya mizunguko ya siku nzima huweza kuingiza Sh40, 000 au kutegemeana na biashara ya siku nzima na siku zote katika matumizi ya fedha amekuwa na tabia ya kuweka akiba ambayo humsaidia siku za mapumziko.
 
Analalamika kuwa kazi kwa sasa imekuwa ngumu kwani magari yamekuwa mengi barabarani na ushindani wa kibiashara umekuwa mkubwa tofauti na zamani.

Kwa upande wake Mage ambaye ni utiongo wa daladala, anasema katika kuifanya kazi yake iwe nzuri, mara nyingi hujitahidi kuwa mkarimu kwa abiria wake
 
lakini kuna baadhi ya watu wamekuwa na maneno ya kuudhi huku baadhi yao kumuambia we msichana unatafuta nini kwenye daladala si bora uende tuu huko ukaolewe.

Malengo

Jenipher anasema malengo yake yeye ni kujua kuendesha gari, kupata leseni ili aweze kuomba kuwa dereva sehemu yoyote na kuachana na kazi ya ukondakta.
 
Kama ulivyoona hapa nimegeuza gari na sikuwahi kufundishwa na mtu bali nimekuwa nikimuangalia dereva anavyofanya na kuamini kuwa naweza na ninashukuru Mungu hata nilipoomba nafasi ya kujaribu dereva wangu aliniruhusu niwe nageuza gari kila tunapofika stendi,” anasema Jenipher.
 
Anasema kitu kinachomsukuma kuendelea kupambana ni pindi anapoona wanawake wenzake wakiendesha magari makubwa ya kwenda mikoani hata kusafirisha mizigo, lakini pia makondakta kutotambuliwa na waajiri wa magari wanayofanyia kazi.
 
Katika kazi hii hata mwajiri hamtambui utingo kama mfanyakazi. Sisi hatupewi mshahara kama madereva na muda wote tunategemea posho,” alisema Jenipher.

Makondakta wanaume

Baadhi ya makondakta wanaume waliowahi kufanya kazi na wanawake wanasema hawaangalii jinsia bali utendaji kazi wa mtu ndio unaweza kuonesha kuwa anafaa au hafai.
 
Kondakta wa daladala Ndolimana Kaduguda anasema wanawake ni watu wanaojali na kuthamini kazi wanapoipata na kutotaka kuichezea.

“Kikubwa tunachoangalia sisi ni uwezo wa kuita abiria akifika stendi, uwezo wa kuchukua nauli. Wote tunarudi nyumbani saa 5.00 usiku na kuamsha gari saa 9.00 usiku kwa hiyo hakuna sababu ya kuwaona tofauti ikiwa wote tunaweza kufanya vitu sawa,” anasema Kaduguda.
 
Jamii inasemaje

Rachel George anasema kondakta mwanamke jamii humchukulia kuwa mtu alieshindikana na kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wake, lakini kwa mtazamo chanya hawa ni wanawake wenye ndoto za mafanikio na walitamani kuwa watu fulani katika jamii lakini ikishindikana kwa sababu mbalimbali ikiwamo kukatishwa tamaa.
 
Jamii inasemaje

Rachel George anasema kondakta mwanamke jamii humchukulia kuwa mtu alieshindikana na kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wake, lakini kwa mtazamo chanya hawa ni wanawake wenye ndoto za mafanikio na walitamani kuwa watu fulani katika jamii lakini ikishindikana kwa sababu mbalimbali ikiwamo kukatishwa tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…