Kuna wanawake wangapi wanaouza miili barabarani na wangapi wanajipatia kipato kwa njia za udanganyifu na tunaishi nao katika jamii? Sasa kwa nini hawa walioamua kujipatia kipato kwa njia halali jamii ishindwe kuwaheshimu kama wafanyakazi wengine,” alisema Rachel.
Albetina Nzyungu mwanafunzi wa kidato cha tatu anasema makondakta wanawake ni watu wenye huruma kwani mara nyingi hujisikia vibaya pindi wanapoacha wanafunzi kituoni.
Makondakta wanaume huwa hawapendi kupandisha wanafunzi hasa nyakati za asubuhi na jioni kwa kuwa tunalipa nauli ndogo, lakini makondakta wanawake huwa hawajali na hata ukikosa nafasi huwaomba watu wasogee ili uweze kuingia,” alisema Albetina.