Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[HASHTAG]#Nigeria[/HASHTAG] Hali si nzuri kwa P-Square kufuatia Peter Okoye kuachilia clip mitandaoni ikionyesha akitukanwa matusi ya nguoni ofisini na kutaka kupigwa na pacha wake na kaka Yao ambaye Ni manager wao kwa muda mrefu. Peter ameenda kwa mwanasheria akitaka kila mmoja apambane na Hali yake kuanzia sasa. Kwa upande mwingine media na mastaa mbalimbali nchini humo wamesikitishwa na mtifuano mkubwa wa mastaa hao waliowahi kutamba Sana Africa na kutaka wayamalize - 5 h
 
Kidole tumbo au Apendeksi hupatikana katika utumbo mkubwa, urefu wake ni kama kidole cha mwisho cha mkono, huwa hakina kazi yoyote mwilini. Sehemu hii hupitisha myeyuko wa chakula na endapo katika chakula hicho kuna michanga au vitu vidogovidogo vigumu, hujikita humo na kushindwa kutoka.

Kidole tumbo pia kinapatikana upande wa kulia wa tumbo kutoka usawa wa kitovu na nyonga ya kulia.
 
Taka ngumu hizo zikishajikita kwenye kidole tumbo na kushindwa kutoka ndipo kinapoanza kuvimba, hali hii kitaalam huitwa ‘Inflammation’. Hapa kidole tumbo kinavimba na kuwa na maumivu na pia hupata maambukizi ya bakteria.
 
Dalili za ugonjwa

Mgonjwa huanza kuhisi maumivu ya tumbo kuanzia usawa wa kitovu ambayo huwa makali na kuacha kisha kusambaa taratibu kuelekea upande wa kulia.

Baada ya muda mgonjwa huanza kutapika kisha kupata homa. Dalili hizi huwa haziji pamoja, huanza moja na kufuata nyingine lakini mgonjwa akiwahi kupata tiba dalili nyingine haziendelei. Baada ya hapo mgonjwa hupata homa.
 
Dalili za ugonjwa zinatofautiana kufuatana na aina ya ugonjwa huu ambapo kawaida umegawanyika katika hali ya ukali ‘Acute’ na hali ya usugu ‘chronic’. Maumivu makali yanayoambatana na homa na kutapika tunaita ni ‘Acute’

Maumivu ya ugonjwa huu ukifikia hatua mbaya husambaa hadi katika uti wa mgongo usawa wa kitovu au ‘Belly button’.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…