Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

“Kutumia dawa bila maelekezo kunaweza kusababisha madhara kama mapunye, vipele kulingana na ngozi ya mtumiaji, hivyo ni hatari kutumia sabuni zenye dawa bila kufahamu nani anatakiwa kutumia na kwa kutibu nini,” anasema Dk Ikeji. Anaeleza kila sabuni inatengenezwa kwa mchanganyiko wake kwa madhumuni ya kutibu kitu fulani, hivyo ni ngumu kutambua madhara au faida anayopata mtumiaji, bila kuangalia kilichomo na kupima aina ya ngozi yake.
 
Mganga mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Leslie Mhina anasema sabuni kama itatumika kutibu maradhi fulani mwilini ni sawa, lakini ikitumika kama pambo ni kuutia mwili usugu endapo utahitaji matibabu ya sabuni hiyo haitafanya kazi kama dawa maana mwili utakuwa umeshaizoea. Anafafanua kuwa, kitu chochote kilichotayarishwa kwa ajili ya kutibu, kitumike kama dawa na siyo vinginevyo.
 
Kutumia dawa kwa kujifurahisha ni kuharibu mfumo mzima wa mwili kutibiwa na dawa hiyo linapotokea tatizo kwani mwili utakuwa umeizoea, ” anasema Mhina.

Mhina anaeleza kuwa ni muhimu pia watumiaji wa sabuni hizo wakasoma maelezo ili kujiridhisha kama inafaa kutumiwa kwa matumizi ya kawaida au ya dawa pekee.
 
Anaeleza kuwa lakini kama mchanganyiko wake hauna kemikali zenye nguvu unaweza usilete madhara yoyote, isipokuwa mtumiaji akipata tatizo la ngozi anaweza asipone akitumia sabuni hiyo kama dawa kwa kuwa mwili utakuwa umeshaizoea.
 
Bangi anafafanua kuwa kama mtumiaji ana mzio wa mchanganyiko uliopo kwenye hizo sabuni, italeta shida sana kwani wengi wao watakuwa hawafahamu kama ni dawa. “Inaweza kuleta tatizo iwapo mtumiaji ana mzio wa kitu fulani halafu kikawemo kwenye moja ya hizo sabuni, hapo ndiyo tatizo litakuwa kubwa anaweza kupata mapunye, kuvimba , kutoka vipele vidogovidogo, tofauti na hapo anaweza asione madhara yoyote,” anasema Bangi.
 
Anaeleza kuwa matumizi yake ni kujikinga na vijidudu kama bakteria, kujikinga na harara, muwasho kama wa joto, hivyo hakuna haja ya kuzuia zisiuzwe mitaani. “Zingesajiliwa kama dawa tungezizuia kuuzwa kiholela, lakini hizi zimesajiliwa kama vipodozi ndiyo maana hatuoni sababu ya kuzizuia kuuzwa maeneo hayo,” anasema Simwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…