Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pole sana mkuu. Nayahisi maumivu yako katika posts zako. Guess what? Huyo aliyekuumiza huko aliko si ajabu hakumbuki na anafurahia maisha yake wakati wewe ungali unateseka. Kibaya zaidi huyo mtu humjui na yeye hakujui. Huoni kama vile unajiumiza bure tu?

Ulishawahi kwenda jukwaa la siasa? Vipi siku ukitukaniwa mama yako? Mitandao hii inawapa watu ujasiri wa ajabu na wala hawafikirii mara mbili kuhusu madhara ya maneno na matusi yao. Kuna negativity kubwa sana huku mtandaoni na ili kuishi vizuri ni lazima kutafuta njia ya kupambana nayo bila kuathirika kisaikolojia. Vinginevyo ni bora hata kutojihusisha nayo kwa sababu utangamano wa kisaikolojia na utulivu wa ndani ni muhimu zaidi kuliko vurugu hizi za mtandaoni.

Anza pole pole kutochukulia matusi na ujinga huu wa mtandaoni kama personal attacks on your being and character bali ni tabia za jumla tu za binadamu hasa wanapopata uhuru huu wa bandia wa mtandaoni. Na pole pole endelea kujitenga na matusi hayo na kuwaepuka watu unaowajua kuwa ni wadhaifu kisaikolojia kiasi kwamba wanategemea kudogosha na kutukana/kuumiza wengine ndiyo wapate farijiko na ridhiko la nafsi. Watu wana mizigo mizito wanatembea nayo na mara nyingi matusi haya wanayoporomosha mitandaoni kwa watu wasiowajua ni kiashiria dhaifu tu cha matatizo yao ya kisaikolojia na kifikra waliyobeba; na anayetukanwa ni target tu isiyo na makosa. Ndiyo maana wakati mwingine mtu anaweza kuanza kukushambulia tu bila sababu maalum.

Baada ya hapo utaona imeanza kuwa rahisi na maumivu hutayasikia tena; na actually watukanaji hawa utaanza kuwaonea huruma na hata kuwaombea. Na mtu akikutukana wala huna haja ya kumtukana pia. We mwambie tu asante mkuu halafu mwombee na nenda zako. Na akiendelea kukufuatilia, mwepuke tu. Pengine akizidi sana ndiyo unaweza ku take a stand. Hata ukifanya hivyo, fanya kwa upendo na epuka kujibu kwa matusi pia. Lakini ukiumia na kuanza kususia thread basi hapo unazidi kushindilia moto wa ego zao na unawapa furaha na ushindi katika mioyo yao isiyo na huruma.

Huwa nasaidia saidia watu ambao huwa bullied humu mitandaoni na kama utahitaji mjadala zaidi kuhusu mada hii niandikie tuendelee kuzungumza zaidi. Huwa sitozi pesa. This is just a psychological game na ni hatari kwa sababu wengine huumia sana na hata kujitoa uhai kisa eti wametukanwa mtandaoni.

Usimpe mtu ye yote nguvu ya kukunyang'anya furaha na amani yako ya kuishi maisha yako unavyotaka as long as huvunji sheria. Mungu Anakupenda na Amekupa kila kitu. Kwa nini unakiruhusu kibinadamu kingine tena usichokifahamu kiingilie amani yako ya moyo?

Mungu Akubariki mkuu...[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]

Aisee Big Brother, your kindness is overwhelming...!!
Kwel kabisaa i should be charged for this but you have given it for free..!
Mkuu kama nilivyomwepesi kuudhika ndivyo pia nilivyomwepesi kuguswa na ishara za kujaliwa na mtu fulani...! Mkuu unaweza ukahisi what you have given me ni kidogo but just taking your precious time kuandika maneno yote haya yaliyojaa ishara za upendo yanamaana kubwa sana kwangu....! Mkuu umenigusa sana sana sana sana katika moyo wangu...! sitosahau busara hizi ndicho ninaweza ahidi na kuwa wakala wa usambazaji wa busara hizi endapo itahitajika..! Barikiwa sana sana sana sana..!!

I have taken notes...!

Usimpe mtu ye yote nguvu ya kukunyang'anya furaha na amani yako ya kuishi maisha yako unavyotaka as long as huvunji sheria. Mungu Anakupenda na Amekupa kila kitu. Kwa nini unakiruhusu kibinadamu kingine tena usichokifahamu kiingilie amani yako ya moyo?
 
Aisee Big Brother, your kindness is overwhelming...!!
Kwel kabisaa i should be charged for this but you have given it for free..!
Mkuu kama nilivyomwepesi kuudhika ndivyo pia nilivyomwepesi kuguswa na ishara za kujaliwa na mtu fulani...! Mkuu unaweza ukahisi what you have given me ni kidogo but just taking your precious time kuandika maneno yote haya yaliyojaa ishara za upendo yanamaana kubwa sana kwangu....! Mkuu umenigusa sana sana sana sana katika moyo wangu...! sitosahau busara hizi ndicho ninaweza ahidi na kuwa wakala wa usambazaji wa busara hizi endapo itahitajika..! Barikiwa sana sana sana sana..!!

I have taken notes...!

Usimpe mtu ye yote nguvu ya kukunyang'anya furaha na amani yako ya kuishi maisha yako unavyotaka as long as huvunji sheria. Mungu Anakupenda na Amekupa kila kitu. Kwa nini unakiruhusu kibinadamu kingine tena usichokifahamu kiingilie amani yako ya moyo?
Anaitwa SYB ni MTU wa busara sana..[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Back
Top Bottom