Kwa upande wa mpunga kama utaondolewa ganda lake gumu la nje na bila kuungarisha, mchele huo kwa kimombo utaitwa "brown rice". Na kama utangarishwa zaidi unatitwa "polished rice".
Hivyo ifahamike kuwa kukoboa kunapoteza kiasi fulani cha unga. Pili, unga usiokobolewa una kiasi kikubwa cha mafuta, protini, madini, vitamini, na nyuzinyuzi (fibre). Kwahiyo, unaimarisha zaidi lishe ya mlaji.
Unga uliokobolewa ni rahisi kuupika. Pumba zinazotokana na kukoboa nafaka zinaweza kutumika kwa kulisha mifugo, kuzalisha nishati, kutengeneza mbolea na matumizi mengine.
Madini ya chuma na zinc yaliyomo kwa wingi katika nafaka mbambali yanaweza kutumika kwa kiwango kikubwa na mwili kama mtu atakula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa.
ÑHii ni kwa sababu nafaka zina kemikali inayoitwa "phytate" ambayo inauzuwia mwili kunyonya madini hizo na kutumika mwilini. Ukikoboa nafaka kama vile mahindi unapunguza kiasikibwa cha kemikali hiyo ya "phytate".
Kwa maelezo ya hapo, ni dhahiri kuwa kukoboa nafaka kuna faida na hasara zake. Tumeona kuwa ukikoboa nafaka kama vile mahindi unapoteza baadhi ya virutubisho kama vitamin, madini na nyuzi nyuzi.
Inashauriwa kwa mtu anaekula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa ale na matunda na mboga za majani za kutosha ili kuziba pengo la vitutubisho vilivyopotea wakati wa kukoboa.
Inashauriwa kwa mtu anaekula chakula kilichopikwa kutokana na unga uliokobolewa ale na matunda na mboga za majani za kutosha ili kuziba pengo la vitutubisho vilivyopotea wakati wa kukoboa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.