Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Asili ya mbawa za ndege huyu ni rangi nyeupe, ila utakapo mchunguza vizuri na kwa utulivu utagundua ana rangi mbalimbali kwenye mbawa zake.
Kichwani ana manyoa marefu yaliyo tengeneza umbo la taji yenye rangi ya dhahabu.
 
Asili ya mbawa za ndege huyu ni rangi nyeupe, ila utakapo mchunguza vizuri na kwa utulivu utagundua ana rangi mbalimbali kwenye mbawa zake.
Kichwani ana manyoa marefu yaliyo tengeneza umbo la taji yenye rangi ya dhahabu.
 
Upande wa kulia na kushoto mwa uso ana rangi nyeupe ambazo kwa juu ya weupe huu kuna vifuko vyenye rangi nyekundu ya kung’aa.
Ana mdomo mfupi wenye rangi ya kijivu na miguu yenye rangi nyeusi.
Nivigumu kumtofautisha dume na jike, japo dume huonekana mkubwa kidogo kuliko jike.
Korongo-taji kijivu wadogo huwa na rangi ya kijivu iliyo kolea zaaidi kuliko wakubwa.
 
MUHIMU KUJUA

Jamii ya ndege hawa ina heshima ya kuwa ndege wa Taifa wa nchi ya Uganda na pia ni moja ya alama katika bendera ya Taifa la Uganda.
Ndege hawa husemekana kuwa hawana usaliti katika mahusiano. Yaani dume hawezi kuwa na jike zaidi ya mmoja hali kadhalika kwa jike pia hawezi kuwa na dume zaidi ya mmoja. Kamwe hawasalitiani na hakuna michepuko. Woowwww “MAPENZI MUBASHARA”
 
MAENEO WAPATIKANAYO KORONGO-TAJI KIJIVU

Ndege hawa wana patikana sana maeneo ya Savana kavu kusini mwa jangwa ka Sahara na hutengeneza viota maeneo yenye maji maji kidogo na aridhi oevu. Mfano wa nchi ambazo ndege hawa huonekana sana tena kwa urahisi ni Uganda, Kenya, Tanzania, Namibia, Rwanda, Msumbiji na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 
Hapa nchini Tanzania Koongo-taji kijivu huonekana zaidi maeneo ya Kaskazini mwa nchi hususani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro.

CHAKULA

Chakula kikubwa cha ndege hawa ni wadudu na wanyama jamii ya tambaaji. Japo kuna wakati hula mpaka mamalia wadogo wadogo kama panya.
 
KUZALIANA

Kabla ya kupandana ndege hawa huanza kucheza na kurukaruka huku kila mmoja akionesha kumvutia mwenzake. Michezo hii huambatana na au kwenda sawia na sauti nzuuri ambazo husababisha muonekano wa kutanuka na kusinyaa kwa fuko la hewa lenye rangi nyekundu linalo onekana maeneo ya shingoni.

Mara tu baada ya kupandana ndege hawa hujenga kiota kwenye maeneo yenye majani marefu au miti mirefu sana iliyo karibu na maeneo yenye aridhi oevu.
 
Jike hutaga mayai mawili mpaka matano (2-5). Jukumu la kutamia mayai huwa ni la wote kwa pamoja kati ya dume na jike na mayai hutotolewa baada ya siku ishirini na nane mpaka thelathini na moja (28-31) yaani takribani mwezi mmoja.

Watoto wa Korongo-taji kijivu huanza kuruka baada ya siku 56-100 japo bado kwa wakati huu huwa wapo chini ya uangalizi wa baba na mama. Kongoro-taji kijivu huishi kwa takribani miaka ishirini au na zaidi.
 
UHIFADHI

Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya ndege hawa kwa sasa ni kati ya 26,500-33,500. Na kati ya hao idadi ya Korongo-taji kijivu wakubwa ni kati ya 17,700-22,300 na walio salia ni watoto.
 
Utafiti uliofanywa na shirika la umoja wa mataifa linalo shughulika na uhifadhi wa maumbileasili duniani (International Union fo Conservation of Nature-IUCN) umebaini kuwa idadi ya ndege hawa imepungua kwa asilimia kubwa sana kutoka 100,000 hadi kati ya 50,000-64,000 toka mwaka 1985-2004. Hii inaonesha kuwa kuanzia mwaka 1985-2004 ndege hawa walipungua kwa asilimia 50% ndani ya myaka 19.
 
Kama hali itaendelea kubaki hivi hawa ndege wanaweza kutoweka kabisa duniani ukizingatia ni ndege ambao wanapatikana barani Afrika tu. Hivyo kutokana na wasiwasi huu ndege hawa wamewekwa katika kundi la wanyama walio kwenye tishio.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKUMBA KORONGO-TAJI KIJIVU

Japokuwa ndege hawa bado wanaonekana baadhi ya maeneo mengi ila wamekua wakikumbwa na changamoto mbalimbali kama zifuatazo hapa chini.
 
Upungufu au kuongezeka kwa mikondo ya maji hasa kwenye maeneo ya mazalia ya ndege hawa hivyo kusababisha kupungua kwa kasi ya kuzaliana.
Kiwango kikubwa cha mifugo na baadhi ya wanyama walao majani kwani huaribu sana maeneo ya mazalia ya Korongo-taji kijivu.
Watoto wa Korongo-taji kijivu kuna wakati huwa wanaliwa na ndege walao nyama kama mwewe na tai lakini hata pia nyoka wakubwa wakubwa.
 
Matumizi ya sumu hasa kwa upande wa wakulima wamekuwa wakiweka sumu yakuwauwa ndege hawa kwani wanadai wamekuwa wakiharibu mazao yao. Mfano mzuri ni hapa kwa majirani zetu wa Kenya ndege hawa wamekuwa wakiuwawa sana kwa sumu mashambani.
 
df1d9e4ca7083c15c732231a350868b4.jpg
 
Uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu katika maeneo ya hifadhi. Mfano mzuri ni uchimbaji wa makaa ya mawe nchini Afrika Kusini umeharibu sana makazi ya ndege hawa.
Ujangili ulio kithiri katika maeneo ya hifadhi na nje ya maeneo ya hifadhi kumesababisha kupungua kwa ndege hawa.
 
NINI KIFANYIKE KUWANUSURU KORONGO-TAJI KIJIVU HUSUSANI HAPA KWETU TANZANIA

Kupambana na uharibifu wa mifereji au mito inayo tiririsha maji katika maeneo oevu wanapoishi ndege hawa.
Kupambana na uharibibu wa mazingira hususani ukataji miti hovyo na nyasi hasa maeneo yanayo zunguka hifadhi zetu.
 
Back
Top Bottom