Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakuna ambaye hajui kuwa wakati mwingine unavokunywa maji unajisikia Amani hata kama ulikuwa na msongo wa mawazo ukichukua glasi moja ya maji ya kunywa unajisikia kama umetua mzigo mkubwa sana katika mwili wako, na hapo ndio utatambua umuhimu wa kunywa maji kuliko kunywa kahawa au soda
 
Lakini cha kushangaza ni kuwa watu wengi hatunywi maji ya kutosha yanayohitajika katika miili yetu na badala yake tunakunywa vimiminika ambavyo kwa namna moja ama nyingine havitusaidii kitu ndani ya miili yetu badala yake vinatusababishia baadhi ya magonjwa ambayo tungeweza kuyaepuka kwa kunywa maji ambayo hayana gharama yoyote ile.
 
BAADHI YA DALILI ZA KUTOKUNYWA MAJI YA KUTOSHA

· MIDOMO KUKAUKA
Hii inaonekana ni kawaida sana lakini kiuhalisia midomo yako inavokauka jua kabisa hauna maji ya kutosha mwilini mwako unachotakiwa ni kuchukua glasi yako ya maji na kunywa kamwe usikimbilie kunywa vimiminika vyenye sukari kwani havitamaliza tatizo lako kwa muda mrefu badala yake baada ya muda mfupi utajikuta hali ya kukauka kwa mdomo inajirudia, lakini ukinywa maji unakuta hiyo hali inaondoka na kuacha mdomo wako ukiwa na unyevu wa kutosha pamoja na mate mdomoni hayatakauka.
 
Screenshot_2017-10-02-19-38-39.png
 
NGOZI KUKAUKA
Ngozi ni kiungo muhimu sana katika mwili wako na inatakiwa ngozi kuwa na unyevu muda wote na sio kavu, ukiona una ngozi iliyokauka jua kwamba haunywi maji ya kutosha na cha kufanya ni kuanza kunywa maji haraka iwezekanavyo ili kuiweka ngozi yako katika hali nzuri ya kuvutia pamoja na unyevu lakini pia kujiweka mbali na magonjwa mbalimbali.
 
NGOZI KUKAUKA
Ngozi ni kiungo muhimu sana katika mwili wako na inatakiwa ngozi kuwa na unyevu muda wote na sio kavu, ukiona una ngozi iliyokauka jua kwamba haunywi maji ya kutosha na cha kufanya ni kuanza kunywa maji haraka iwezekanavyo ili kuiweka ngozi yako katika hali nzuri ya kuvutia pamoja na unyevu lakini pia kujiweka mbali na magonjwa mbalimbali.
 
MMENG’ENYO WA CHAKULA KUTOFANYA KAZI VIZURI
Usipokunywa maji ya kutosha mmeng’enyo wa chakula hauwezi kufanya kazi yake vizuri kwani maji husaidia chakula kisagike vizuri tumboni, na chakula kisiposagika vizuri utashuhudia kuwa unapata matatizo ya tumbo ambayo yatasababisha ushindwe kwenda haja kubwa vizuri na wakati mwingine utaenda haja kubwa kwa kutumia nguvu nyingi pamoja na kuumia, ili kuepuka yote hayo na kuiweka afya yako katika hali nzuri hunabudi kunywa maji yakutosha.
 
KUPATA KIASI KIDOGO CHA HAJA NDOGO
Amini usiamini usipoenda haja ndogo mara nne mpaka saba kwa siku jua kabisa kiwango cha maji kilichopo mwilini mwako ni kidogo sana na hata ukienda basi haja ndogo inatoka kidogo sana huku ikiwa na rangi ya njano, hali hiyo ikiendelea itakusababishia magonjwa ambayo yanaweza kuepukika kwa kunywa maji tu.
 
Mimi najitahidi kunywa maji kila wakati na ninaona matokeo yake mazuri kwa kujiweka mbali na magonjwa mbalimbali kwani maji ni tiba muhimu sana na yanatibu magonjwa mengi bila kujua na kitu kizuri ni kuwa maji hayana gharama yoyote ile kwa hiyo hata wewe unaweza kuanza sasa kujiwekea utaratibu wa kunywa maji kadiri unavyoweza na ninakuhakikishia kuwa utapata matokeo mazuri na hautajutia maamuzi yako ya kunywa maji.
 
Back
Top Bottom