Magonjwa ya zinaa ni magonjwa yanayoambukizwa hasa kwa kujamiiana. Magonjwa haya hayana lika wala jinsia yana weza kumwathiri mtu yeyote mwenye kuweza kujamiana na mtu ambaye amekwisha ambukizwa magonjwa hayo.
Magonjwa haya mpaka sasa yanayoweza kuambukizwa kwa kujamiana ni kama UKIMWI, kisonono, kaswende, klamydia, pangusa, kabambala, malengelenge, Trichomoniasis, viota, utando.
Tukiachana na UKIMWI naomba kuzungumzia magonjwa haya mengine ya zinaa.
Magonjwa haya huanzia sehemu za siri kama matibabu hayatapatikana ya haraka huweza kusambaa katika sehemu nyingine ndani ya mfumo wa uzazi. Hapo huwa hatari kwa mgonjwa kwani hali hiyo huweza kumpelekea kupoteza uwezo wake wa kupata mtoto.
Magonjwa kama kaswende huu unauwezo wa kuathiri mwili mzima, yanapokosa matibabu ya haraka husambaa sehemu nyingine za mwili kwa damu na kwenda kuathiri maeneo mengine ya mwili kama mapafu na hata kuweza kusababisha kifo.
Bila kusahau saratani ya kizazi hasa kwa wanawake saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia kubwa husababishwa na magonjwa haya zinaa hasa HPV, hivi ni virusi ambavyo vinasambaba kwa kujamiana bila kinga.
Magonjwa kama kisonono hili ni hatari sana kwa wanawake kuliko wanaume, kwani kwa mwanaume ni rahisi sana kugundua kama ameambukizwa kisonono tofauti na mwanamke. Kwa mwanaume uchukua siku 2 kuweza kugundua kwa kutoka majimaji kama usaa sehemu za siri.
Kwa wanaume ni vizuri unapogundua dalili za awali za magonjwa ya zinaa usisite kwenda kituo cha afya na mpenzi wako, kwa kufanya hivyo utakua umeokoa watu wengine kuathirika na ugonjwa huo pia utakua umemsaidia mwenzi wako kupatiwa matibabu mapema kwani kwa mwanamke sio rahisi kupata dalili za ugonjwa huo mapema kama kwa wanaume.
Kwa wanaume ni vizuri unapogundua dalili za awali za magonjwa ya zinaa usisite kwenda kituo cha afya na mpenzi wako, kwa kufanya hivyo utakua umeokoa watu wengine kuathirika na ugonjwa huo pia utakua umemsaidia mwenzi wako kupatiwa matibabu mapema kwani kwa mwanamke sio rahisi kupata dalili za ugonjwa huo mapema kama kwa wanaume.
Huongeza hatari hasa kwa wamama wajawazito, inaweza kusababisha mimba kutoka au kujifungu mtoto kabala ya miezi tisa (mtoto njiti) au kujifungua mtoto akiwa na ulemavu wa viungo.
Hatari nyingine ya magonjwa haya ya zinaa ni mgusano tu, yani uaweza kuambukizwa kwa kugusana sehemu za siri na mtu aliekwisha ambukizwa tofauti na UKIMWI yani damu kwa damu.
Mzio au kwa lugha ya kigeni ni unaweza kusema allergy.
Kwa kawaida mwili unapohisi kuna kitu kigeni kimeingia ndani ya mwili mfano vumbivumbi au madawa na chemikali nyinginezo, kinga ya mwili huzalisha antibodies ambazo huenda kuondoa vitu hivyo kusudi visilete madhara ndani ya mwili.