Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Moyo ni kiungo cha mwili chenye kazi kubwa ya kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili wako.
Moyo umeundwa na misuli yenye uwezo wa kutanuka na kusinyaa mara kwa mara bila kuchoka na hufanya kazi yake katika kipindi chote cha maisha ya binadamu.
 
Moyo umegawanyika katika sehemu 2;
1. Sehemu ya kushoto ya moyo
2. Sehemu ya kulia ya moyo

Pia sehemu hizo mbili kila moja imegawanyika katika vyumba viwili, auriko na ventriko.
Hivyo basi moyo wa binadamu unakua na vyumba vinne kwa ujumla.
 
Auriko hufanya kazi ya kupokea damu na kuiruhusu kuingia kwenye ventriko na ventriko hufanya kazi ya kuisukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili. Mfano ventriko ya kulia hufanya kazi ya kusukuma damu kwenda kwenye mapafu na auriko ya kushoto upokea damu kutoka kwenye mapafu.
 
Moyo unauwezo wa kusukuma damu katika katika kasi tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Mwili unapokua una uhitaji mkubwa wa oksijeni na virutubisho vingine vya mwili husababisha moyo kusukuma damu kwa kasi kubwa hivyo husababisha mapigo ya moyo kwenda kwa kasi. Mfano mtu anapofanya mazoezi au anapofanya kazi nzito mwili wake huwa na mahitaji makubwa ya oksijeni na kufanya moyo kusukuma damu kwa kasi.
Mwili utakapokamilisha mahitaji yake moyo hurudi katika kasi yake ya kawaida.
 
Tuanze kuwaangalia hawa anbao hawana madhara katika mwili.
Mwili wako unakutana na bakteria wengi na wa aina mbalimbali katika maisha yako ya kila siku unayoishi, huweza kupata kwa kuvuta hewa, kula chakula pia kwa kugusana.
 
2141.jpg
 
Back
Top Bottom