Moyo ni kiungo cha mwili chenye kazi kubwa ya kusukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili wako.
Moyo umeundwa na misuli yenye uwezo wa kutanuka na kusinyaa mara kwa mara bila kuchoka na hufanya kazi yake katika kipindi chote cha maisha ya binadamu.
Auriko hufanya kazi ya kupokea damu na kuiruhusu kuingia kwenye ventriko na ventriko hufanya kazi ya kuisukuma damu kwenda sehemu mbalimbali za mwili. Mfano ventriko ya kulia hufanya kazi ya kusukuma damu kwenda kwenye mapafu na auriko ya kushoto upokea damu kutoka kwenye mapafu.
Moyo unauwezo wa kusukuma damu katika katika kasi tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya mwili. Mwili unapokua una uhitaji mkubwa wa oksijeni na virutubisho vingine vya mwili husababisha moyo kusukuma damu kwa kasi kubwa hivyo husababisha mapigo ya moyo kwenda kwa kasi. Mfano mtu anapofanya mazoezi au anapofanya kazi nzito mwili wake huwa na mahitaji makubwa ya oksijeni na kufanya moyo kusukuma damu kwa kasi.
Mwili utakapokamilisha mahitaji yake moyo hurudi katika kasi yake ya kawaida.
Bakteria ni kiumbe hai kidogo ambacho huwezi kukiona kwa macho. Bakteria ni kiumbe hai chenye seli moja. Bakteria wapo wengi wa aina mbali mbali na hupatikana katika mazingira mbalimbali.
Tuangalie hawa bakteria wanaopatikana katika mwili binadamu.
Hawa bakteri wanaopatikana katika mwili wa binadamu tunaweza kuwaweka katika makundi mawili kama;
Kuna bakteria waletao madhara na
Kuna bakteria ambao hawana madhara.
Tuanze kuwaangalia hawa anbao hawana madhara katika mwili.
Mwili wako unakutana na bakteria wengi na wa aina mbalimbali katika maisha yako ya kila siku unayoishi, huweza kupata kwa kuvuta hewa, kula chakula pia kwa kugusana.
Mfano wa bakteria hawa ambao hawana madhara katika mwili hupatika na kwenye utumbo mpana na bakteria hawa huusadia mwili katika shughuli zake za kumeng’enya chakula.
Pia kuna baadhi ya bakteria hupatikana katika sehemu za siri za mwanamke, bakteria hawa hutengeneza asidi ya uke hivyo kuufanya uke kujilinda na maambukizo ya bakteria na wadudu wengine wanoweza kusababisha madhara katika mwili.
Pia tuangalie kundi lingine la bakteria ambao husababisha madhara katika mwili. Bakteria hawa wana uwezo wa kuusababishia mwili madhara pindi watakapo pata nafasi ya kuingia ndani ya mwili.