Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ndani ya seli nyekundu za damu protini inayoitwa himoglobini inapatikana kwa wingi.
Himoglobini ina madini ya chuma ambayo husaidia katika usafirishaji wa gesi ya oksijeni kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Himoglobini hukamata oksijeni mahali ambapo kuna mkusanyiko wa oksijeni nyingi kama kwenye mapafu na kuziachilia pale inapofika mahali ambapo oksijeni ni chache.
 
Pia plasma husafirisha taka mwili kutoka sehemu mbalimbali za mwili na kuzipeleka katika sehemu zinapohitajika kwa ajili ya kutolewa nje ya mwili. Mfano. Taka mwili nyingi katika mwili husafirishwa ndani ya plasma na kupelekwa katika figo ambapo hutolewa nje kwa njia ya mkojo.
 
Kwa mfano homoni ya Insulini hutengenezwa kwenye kongosho. Baada ya kuzaliswhwa huingia moja kwa moja kwenye damu na kusafirishwa kwenda sehemu mbalimbali za mwili kwa ajili ya kudhibiti kiwango cha sukari mwilini ili mwili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…