Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6). Wabinafsi.

Watu hawa wanajijali wao tu, na hawawajali wengine. Wanaangalia kitu kitakachowanufaisha wao tu bila kuangalia kama kina madhara kwa wengine. Watu kama hawa wanapenda kupokea tu, hawapendi kutoa.
 
1507396309569.jpg
 
Rafiki naomba nieleweke hapa, binadamu tumeumbwa na ubinafsi. Kila binadamu ana ubinafsi ndani yake. Lakini ninachoongelea hapa ni ubinafsi ulio na madhara kwa wengine. Yaani unakuta mtu yuko tayari kufanya kitu chochote ajinufaishe yeye tu bila kuangalia madhara kwa wengine. Watu kama hawa waepuke kwenye maisha yako.
 
Watu kama hawa wanaweza wakawa na wewe kama rafiki kwa kukutumia tu wakamilishe haja zao. Wanachoangalia ni faida kwao tu. Watu kama hawa wanachukia sana wakiona wengine wanafanikiwa. Wanapenda wafanikiwe wao tu.

Waweke pembeni watu hawa kwenye maisha yako, kwa sababu ukiwa nao watakutumia tu.
 
7). Watu wasio na malengo na maisha yao.

Hawa ni watu walioridhika na maisha na hawana ndoto yoyote na maisha yao. Watu hawa hawana malengo na maisha yao, wanaishi ilimuladi siku zimeenda.
 
Watu kama hawa hawajisumbii kuwaza wafanye nini kubadili hali zao za maisha. Ni watu ambao wanakubaliana na hali zao za maisha na wanaamini ndivyo walivyo na wanaendelea kuishi hivyo kila siku.
 
Rafiki watu wasio na malengo na maisha yao hawatakupa hamasa yoyote ya kwenda mbele. Na hawa wanaweza kugeuka na kuwa wakatishaji tamaa namba moja kwenye mafanikio yako.
 
Back
Top Bottom