Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watu kama hawa watakufanya na wewe uweke pembeni malengo yako na kukubaliana na hali uliyonayo hata kama ni mabaya. Na utaanza kusema maneno kama ‘haya ndio maisha’, ‘hivi ndivyo maisha yalivyo’, na wakati ungeweza kuisha maisha mazuri zaidi ya hayo. Waepuke watu hawa rafiki kama unataka kufanikiwa
 
1507396300328.jpg
 
8). Wanafiki.

Hawa ni watu ambao wanakwambia hiki, wakikupa mgogo wanasema kingine. Hawa sio watu wa kuwaamini katika mafaniko yako. Ukiwaamini lazima siku moja utaumia. Wanaweza kukwambia kitu leo ukazani ni kweli lakini baadae ukaja gundua ni uongo.
 
Watu kama hawa wanaweza kukuchonganisha na marafiki zako, watu wako wa karibu au mpenzi wako na usipokuwa makini inaweza kuleta mgogoro mkubwa na watu wako wa karibu. Waepuke watu hawa kwenye maisha yako.
 
9). Watu wenye majivuno na wenye kiburi.

Hawa wanajiona wao ni bora sana kuliko wengine. Wanajiona wao wako juu kuliko wengine. Wanapenda kuwaona wengine wako chini yao siku zote. Wakifanikiwa basi mtaa mzima utajua.
 
  • Thanks
Reactions: Soe
Watu hawa ukifanikiwa lazima waumie. Na siku zote wanaamini hakuna mtu aliye bora kuliko wao. Wanawashusha wengine ili wajione ni dhaifu kuliko wao. Kama kweli unataka kufanikiwa, waweke pembeni watu hawa rafiki.
 
10). Wakosoaji.

Hili ni kundi lingine la watu la kuwaepuka. Ndio kukosolewa kupo katika maisha. Tunahitaji kukosolewa ili tuwe bora wakati mwingine. Kama kuna kasoro mtu kaiona na kakwambia haina budi kuingalia na kuifanyikia kazi.
 
Lakini kuna watu wao ni kukosoa tu, hakuna uzuri wowote wanao uona kwa mtu au kitu. Yaani watu kama hawa wanaangalia kasoro iko wapi siku zote. Hata ufanye vizuri kivipi watakukosoa tu. Hata kitu kiwe kizuri kivipi watatafuta kasoro iko wapi, utazani wameumbwa kukosoa tu kwenye maisha yao.
 
“You are the average of the five people you spend the most time with”- Jim Rohn

“Wewe ni wasitani wa watu watano unaokaa nao muda mwingi”.- Jim Rohn Kama unataka kufanikiwa hakikisha unatumia muda mwingi kukaa na watu ambao watakuwa na msaada kwenye mafanikio yako. Waepuke watu wote wanaokurudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom