Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Changamoto ni sehemu ya maisha. Ufanye Mambo mazuri au mabata lazima utapitia changamoto tu. Uwe maskini au tajiri lazima utapitia changamoto. Uwe mwerevu au mjinga lazima utapitia changamoto. Kila mtu anapitia changamoto, sema unaweza tu kuficha watu wengine wasijue lakini changamoto ni lazima. Kuna muda uwa tukiwaona watu wana maisha mazuri tunazani hawana changamoto, lakini ukweli ni kwamba hata wenye maisha mazuri kupitia changamoto ni kitu cha lazima.
 
Sema anayejua kuitumia vizuri pesa, changamoto ya uhuru wa fedha haitakuwa inamsumbua ila asiye na matumizi mazuri pamoja na changamoto zingine changamoto ya uhuru wa kifedha itakiwa inamsumbua.
 
Pesa uwa inamfata mtu ambaye anajua kuitumia na kuizalisha vizuri na uwa inamkimbia kila mtu ambaye hajui kuitumia vizuri na kuizalisha. Ndio maana usipokuwa na matumizi mazuri ya pesa, lazima kila siku utakuwa na matitizo na pesa.
 
Sema anayejua kuitumia vizuri pesa, changamoto ya uhuru wa fedha haitakuwa inamsumbua ila asiye na matumizi mazuri pamoja na changamoto zingine changamoto ya uhuru wa kifedha itakiwa inamsumbua.
 
Rafiki yangu nimeeleza sana kuhusu changamoto. Changamoto ni ugonjwa wa kila mtu. Magonjwa mengine unaweza kuyakwepa lakini sio changamoto.

Unapopita katika changamoto kumbuka kila mtu anazo za kwake. Lengo langu la kukuandikia leo ni kukupa maneno matatu yatakayokusaidia kipindi unapitia changamoto. Maneno yenyewe ni haya hapa nchini rafiki yangu:
 
Imani

Imani ni kuwa na uwakika na jambo unalotarajia. Bila kuwa na imani huwezi kupata matokeo unayotegemea kupata. Na imani siku zote inaenda na matendo, kama kuna kitu unakiamini lazima ukiweke kwenye matendo.
 
Haijalishi unapitia changamoto gani, kama ukiilinda imani yako una uwakika wa kufika unakotarajia kufika. Usipoteze imani yako rafiki yangu unapopita kwenye magumu. Ukipoteza imani tu ujue unakaribisha kuanguka. Endelea kuamini kwamba unaweza kufika unapotaka kufika, endelea kuamini kwamba unayotarajia ipo siku yatatokea, usikate tamaa rafiki yangu. Amini, amini, amini.
 
sania.xo-1.jpg
 
Pambana

Neno la pili nalotaka kukushirikisha rafiki yangu ni kupambana. Yaani rafiki yangu hakuna kitu kizuru uwa kinakuja kirahisi. Historia za watu wengi waliofanikiwa walikuwa ni watu wa kupambana. Waliweka bidii kwenye kile walichokuwa wanafanya kwa sababu wanajua mkono mlegevu uleta umaskini bali mkono wa mwenye bidii uleta mali. Fanya kazi kwa bidii, weka msimamo, pambana mpaka uone matokeo.
 
Fanya tena

Neno la mwisho ni kufanya tena. Kama unapitia changamoto kiasi kwamba umepoteza kila kitu au umeshindwa, jipange upya na rudia tena. Kumbuka kila kwenye kushindwa kuna cha kujifunza. Kushindwa sio mwisho wa maisha rafiki, kushindwa maisha ni kukata tamaa na kutojaribu tena. Kama bado unaishi maana yake ipo nafasi ya wewe kujaribu tena. Kumbuka lakini kurekebisha makosa uliyofanya pale uliposhindwa. Zipo mifano mingi ya watu walioshindwa na wakaweza kunyanyuka tena na kusimama kwa nini wewe ushindwe?

Amini, pambana na fanya tena mpaka uone matokeo.
 
Back
Top Bottom