Haijalishi unapitia changamoto gani, kama ukiilinda imani yako una uwakika wa kufika unakotarajia kufika. Usipoteze imani yako rafiki yangu unapopita kwenye magumu. Ukipoteza imani tu ujue unakaribisha kuanguka. Endelea kuamini kwamba unaweza kufika unapotaka kufika, endelea kuamini kwamba unayotarajia ipo siku yatatokea, usikate tamaa rafiki yangu. Amini, amini, amini.