Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Corrupt power? Says who? Hiyo anarchy anayozungumzia iko wapi? Walifanya nini Wakati Wanyarwanda wanauana wao kwa wao? Tunalishwa hizi propaganda bila kuzichekecha. Tunalazimishwa kufuata hii demokrasia ya Wamarekani ya one size fits all. Mbona imeshindwa kufanya kazi huko Iraq? Mbona imekwama Afghanistan? Mbona Marekani kwenyewe inalega lega?

Demokrasia ni lazima iheshimu utamaduni na historia ya watu pamoja na mila zao. Kufanya vinginevyo ni kujilisha upepo. Na Wamerakani wanaitumia dhana tata ya demokrasia kama kisingizio cha kueneza ubeberu wao. Ndiyo maana Trump akienda Saud Arabia anasema "hatuko hapa kuwafunza jinsi ya kuishi na kuendesha maisha yenu" lakini akienda Iraq anasema tunataka demokrasia. Unafiki mtupu...!!!

Kisingizio cha demokrasia kinapitwa na wakati. Next ni ushoga. Napo tutaona kama tutakubali kuwa mashoga ili kuwaridhisha Wamarekani na dhana yao potofu ya demokrasia. Miafrika haishangazi hata tukifananishwa na manyani na kutupiwa maganda ya ndizi huko viwanjani Ulaya kwa sababu akili yetu ni ya kinyani nyani tu. Sad !!!
 
37cca25286b444b49f5029d027ba1160.jpg
 
Back
Top Bottom