Rais Kenyatta amjia juu Raila Odinga baada ya kutangaza kujitoa
Rais Uhuru Kenyatta amemjia juu Kiongozi wa NASA Raila Odinga baada ya kutangaza kutoshiriki uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya na kusema hata kama amejitoa Katiba ya Kenya haizuia uchaguzi kutofanyika
Kenyatta amesema kuwa Odinga alitaka uchaguzi urudiwe jambo ambalo limeigharimu nchi ya Kenya fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kujenga barabara, zingeweza kutumika kujenga mahospitali na kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, lakini anashangaa mtu ambaye ametaka uchaguzi kurudiwa anajiengua tena.
Siasa uchwara in SYB's voice[emoji23][emoji23]