Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BZORYykgifA.jpg
 
Eneo ulipo kwa wakati husika

Kuna uwezekano unapoweka chapisho (post) mtandaoni likaonyesha pia eneo ulilopo; hii linategemeana na mpangilio wako wa faragha. Pia watu wenyewe wamekuwa wakionyesha wako maeneo gani katika machapisho (post) zao mbalimbali.
 
Hiki si kitu kizuri kwani kinawajulisha watu wabaya ulipo; hivyo wanaweza kwenda kukuibia nyumbani, au ofisini au hata kukuteka kwani wanajua eneo ulilopo. Hivyo ni vyema kubadili mpangilio wako wa faragana (privacy settings), pia kutokuchapisha eneo ulilopo kwa ajili ya usalama wako.
 
Picha za watoto wako au wa jirani

Watu wengi hupenda kuweka picha za watoto kwenye mitandao tena wakiwatagi hata majina. Kwa hakika huwezi kujua ni nani ataziona hizo picha na atazitumiaje. Ulishiwahi kufikiri kama akaunti ya rafiki itaibiwa na mtu mbaya? Piacha unazoziona leo zikitumika katika matangazo, hata yale mabaya si zote zimenunuliwa;
 
Anwani ya mahali unapoishi

Kama ilivyo kwa eneo ulipo kwa wakati husika, si vyema kuonyesha anwani kamili ya mahali unapoishi. Je unajua akaunti yako itaonwa na nani? Inawezekana wahalifu wakakufwatilia kwa kutumia taarifa ulizoweka kwenye akaunti yako. Hatari huzidi kwa wale watu wanaopenda kuonyesha wanaishi maisha ya kifahari nyumbani wakiwa na vitu vya thamani kubwa.
 
Namba yako ya simu

Kama nilivyotangulia kusema katika dondoo zilizotangulia kuwa huwezi kujua taarifa zako zinaonwa na kutumiwa na nani. Epuka kuweka namba yako ya simu kwenye mitandao kwani inaweza kutumia na watu wabaya kufanya uhalifu au hata kukufwatilia.
 
Mahusiano

Watu wengi hupenda kuonesha hali za mahusiano yako kwenye mitandao ya kijamii. Hebu fikiri umeonyesha kuwa uko kwenye mahusiano na mtu ambaye amemwacha mpenzi wake; ni dhahiri kuwa kuna uwezekano huyo mpenzi wa awali akataka kufanya kitu kibaya juu yenu. Hivyo epuka kuweka maswala yako ya mahusiano kwenye mitandao kwani hujui anayeona ni nani na atafanya nini kutokana na taarifa hizo.
 
Safari au mapumziko

Unapoandika kuwa umesafiri au uko kwenye mapumziko, kwa ufupi umesema “Sipo nyumbani au ofisini hivyo mnaweza kufanya chochote”. Kumbuka taarifa kama hizi zitatoa mianya kwa wahalifu watakapoziona. Jitahidi kuweka picha au taarifa kama hizi baada ya safari au mapumziko ili kulinda usalama wako.
 
Back
Top Bottom