Mali na utajiri
Akaunti nyingi za watu hupambwa kwa mali na maisha ya anasa na kifahari. Watu wamekwenda mbali zaidi na kuweka kila kitu walichonacho kwa piacha, maandishi na hata zideo. Nimeshuhudia watu wakiweka magari, nyumba, viwanja, mishahara, kiasi cha matumizi yayo, bei za vitu walivyo navyo n.k. Ulishawahi kujiuliza haya yote ni kwa ajili ya nini? Je ni wote wanaburudishwa na taarifa hizi? Fungua macho; hapa ni sawa na kumpeleka swala katika bunge la simba. Tambua unawajulisha wahalifu palipo na vya kuiba; hivyo ficha maswala yahusuyo mali na utajiri wako katika mitandao ya kijamii.