Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni wazi kuwa sasa kuna ongezeko kubwa sana la matumizi ya simu za mkononi hasa simu za kisasa (smartphone). Ni ukweli usiopingika kuwa yapo matumizi mengi ya simu za mkononi pamoja na programu zake (applications) ambayo bado hayajafahamika vyema kwa watumiaji wake.
 
Google drive ni zaidi ya hazina ya mafaili. Google Drive inakuwezesha kutengeneza ofisi yako ndogo yenye uwezo mzuri wa kuunda, kupanga, kuhariri na hata kusambaza mafaili mbalimbali kadri upendavyo.
 
Android Device Manager

Ukizingatia kwamba simu ni muhimu sana kwenye maisha yetu, tunahitaji kitu cha kutusaidia ikiwa jambo litakwenda vibaya. Android Device Manager itakuwezesha kufanya mambo kama vile kuibaini simu yako utakapo sahau ulipoiweka, kubadili nywila au neno la siri n.k.
 
Avast Mobile Security

Ni vizuri kutambua kuwa usalama ni jambo la kwanza. Kutokana na kuwepo kwa hatari mabalimbali hasa kwa simu zinazotumia Android, ni vyema ukajikinga kwa kutumia Kinga-virusi (antvirus) ya Avast. Avast ni nzuri kwani itakagua mafaili, WiFi, App na hata kuongeza kasi ya RAM ya simu yako.
 
Avast Mobile Security

Ni vizuri kutambua kuwa usalama ni jambo la kwanza. Kutokana na kuwepo kwa hatari mabalimbali hasa kwa simu zinazotumia Android, ni vyema ukajikinga kwa kutumia Kinga-virusi (antvirus) ya Avast. Avast ni nzuri kwani itakagua mafaili, WiFi, App na hata kuongeza kasi ya RAM ya simu yako.
 
Google Maps

Teknolojia imekuwa na imerahisisha maisha. Unaweza kwenda mahali popote sasa kwa kutumia tu mwongozo kutoka kwenye simu yako na kufika bila matatizo. Unaweza kuweka Google Maps kwa ajili ya kujifunza au hata kupata mwongozo wa eneo unalotaka kwenda.
 
Facebook, Snapchat, Instagram, YouTube

Nimekusanya mitandao maarufu ya kijamii pamoja hapa uchague unaoupenda. Kama wewe ni mtumiaji wa Facebook basi pakua app ya Facebook ili uweze kutumia Facebook kwa ubora, urahisi na hata usalama zaidi. Pia unaweza kufanya hivi kwa mitandao yako mingine.
 
Ni wazi kuwa kwa sasa simu ni zaidi ya kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe mfupi. Naamini hutobaki tena nyuma kwenye kutumia simu yako kwa namna yenye tija baada ya kufahamu app hizi. Nikukumbushe kuwa zipo app nyingi sana lakini siyo zote zenye tija kwako;
 
e14bf322d4a4cc3d353c2d77ae0286a4.jpg
 
Back
Top Bottom