Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Manchester City wakiwa wanaandaa dau la paundi milioni 20 kwa ajili ya Alexis Sanchez Januari. AC Milan wanajipanga kumsajili Sergio Aguero, kwa mujibu wa Daily Mail .
Ripoti zinadai kuwa Pep Guardiola yupo tayari kumruhusu Sergio Aguero kuondoka ikiwa atampata Alexis Sanchez.
 
Arsenal wanajipanga kumsajili winga wa Everton Ademola Lookman, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa zamani wa Charlton Athletic amekuwa na wakati mgumu katika Goodison Park licha ya kung'ara kwenye kikosi cha Uingereza U-20 Kombe la Dunia majira ya joto.
 
Luka Modric amekuwa akivujisha taarifa muhimu za Real Madrid kwa bosi wa Manchester United Jose Mourinho, kwa mujibu wa Diario Gol .
Ripoti zinadai kuwa Modric amekuwa akumfahamisha Mourinho kuhusu mambo yanayoendelea kwenye chumba cha kubadilishia nguo Santiago Bernabeu na kuwa Mreno huyo anaweza kutumia taarifa hizo kumnunua Gareth Bale kwa bei pungufu.
 
Southampton wapo tayari kutoa paundi milioni 15 kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott Januari, kwa mujibu wa Daily Express .
Walcott pia yumo kwenye rada za Everton, West Ham na Inter, lakini Southampton wanaamini watafanikiwa kumshawishi Muingereza huyo kurejea St Mary's baada ya muongo mmoja tangu ajiunge na Arsenal.
 
Fenerbahce inafikiria kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi Daley Blind kutoka Manchester United kwa mujibu wa habari kutoka Hurriyet, via Talksport .
Blind anaweza kucheza kama beki wa kati, beki wa kushoto na hata kiungo mkabaji, lakini hana uhakika katika kikso cha Jose Mourinho.
 
Jupp Heynckes baada ya kustaafu atarejea tena kuinoa Bayern Munich mwisho wa msimu huu kwa mujibu wa Bild .
Heynckes mwenye umri wa miaka 72 alishinda mataji matatu akiwa na mabingwa hao wa Ujerumani kabla ya kuwasili kwa Pep Guardiola 2013, na atachukua nafasi ya Willy Sagnol anayeiongoza klabu hiyo kwa muda baada ya Ancelotti kutupiwa virago.
 
Lionel Messi, Neymar na Cristiano Ronaldo wametajwa katika majina ya mwisho kuwania tuzo ya Mchezaji bora wa wa kiume FIFA 2017.
Nyota wa Real Madrid Ronaldo alishinda tuzo ya mchezaji bora mwaka jana.
Paneli itakayomchagua mchezaji bora ni pamoja na Cafu, London Donovan, Enzo Francescoli, Diego Maradona, Carles Puyol, Carlos Valderrama na Edwin van der Sar.
Mshindi atatangazwa London Palladium Oktoba 23.
 
Messi alikuwa wa pili baada ya Ronaldo katika kura za msimu uliopita, Antoine Griezmann akishika nafasi ya tatu.
Nyota wa paris Saint-Germain Neymar alishika nafasi ya nne katika tuzo za FIFA 2016, lakini amepanda tatu bora mwaka huu sambamba na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona Messi.
Kulikuwa na wachezaji 24 katika orodha ya awali, Gianluigi Buffon, Paulo Dybala, Griezmann, Harry Kane, Sergio Ramos na Alexis Sanchez miongoni mwa majina yaliyokatwa kabla ya kupatikana matatu a mwisho.
 
Ronaldo pia anapewa nafasi kubwa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or, na anapigiwa chapuo kutwaa tuzo ya FIFA tena baada ya msimu wa 2016-17 ambao alitwaa ubingwa wa La Liga na Ligi ya Mabingwa akiwa na Madrid.
 
MUME ni kama MWIKO wa kupakulia chakula . Mwenzio akitumia unaoshwa na wewe unautumia kama kawaida . Kwa hiyo hakuna mwanaume MALAYA ila wanaume wote ni BABALISHE tu . Kwa hiyo wewe usiogope na wala usione wivu ukasema "ooh mume wng Malaya !" Hapana .we muulize kwa upole tu. BABALISHE huo mwiko UMEUSUUZA? Maana na Mimi nataka kuutumia . WATUMIE WANAWAKE WOTE WENYE WIVU KWA WAPENZI WAO [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom