Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MAISHA YA PWANI NI SHIDA [emoji38][emoji38][emoji38] [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kula[emoji510] kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwa *UKISUSA WENZIO WALA* ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwa *UKITOKA [emoji124][emoji124]MWENZIO ANAINGIA*[emoji126][emoji126] jamaa akagoma kwenda kazini [emoji51][emoji51] mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwa *NIMEMDHIBITI NDO MANA HATOKI*[emoji730] jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbani kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwa *ULIDHANI RAFIKI YAKO KUMBE ADUI YAKO* jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwa *NI BORA NIMPE JIRANI KULIKO KIOZEE NDANI*
Jamaa yuko ICU!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
"Mwanamke hapigwi kwa ngumi, hupigwa kwa doti ya Kanga"
 
00-lede-jlo.jpg
 
SIMULIZI, MCHAMUNGU NA MFALME MTATA. Kulitokea Mchamungu mmoja kwenye nchi ya Mfalme Bwanga. Mchamungu huyu alikuwa maarufu kwenye mji alioishi mfalme Bwanga. Siku moja Mchamungu alikuwa muhitaji, na hitajio lake hasa lingeweza kutatuliwa na mfalme maana lilihitaji kiasi furani cha fedha. Hivyo Mchamungu akajitosa kwenye jumba la kifalme kuonana na mfalme Bwanga. Baada mfalme kufikishiwa taarifa juu ya ujio wa Mchamungu akaruhusu aingie.
Enandelea....
 
Virutubishi
ni viini vilivyoko kwenye chakula ambavyo vinauwezesha mwili kufanya kazi zake, karibu vyakula vyote huwa na kirutubishi zaidi ya kimoja ila hutofautiana kwa kasi na ubora. Kila kirutubishi kina kazi yake mwilini na mara nyingi hutegemeana ili viweze kufanya kazi yake kwa ufanisi. Hakuna chakula kimoja chenye virutubishivya aina zote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto, ni mhimu kula vyakula vya aina mbalimbali ili kuwezesha mwili kupata virutubishi mchanganyiko vinavyohitajika.
 
Kabohaidreti / vyakula vya wanga
Kabohaidreti / vyakula vya wanga huvipa mwili nguvu inayoihitajika kujiendesha. Vyakula
hivi vyaweza kuwa sahili au changamani. Hii inahusu jinsi ambavyo chakula chaweza
kubadilisha sukari katika mwili. Vyakula vya wanga na sukari huvipa mwili nguvu
inayohitajika kuufanya upumue na kuendelea kuishi, kuwa na mwendo na utoaji joto, na kwa
ukuaji na utengenezaji wa mkusanyiko wa seli (tishu). Baadhi ya wanga na sukari
hubadilishwa kuwa mafuta mwilini.
Ufumwele utokanao na kabohaidreti hufanya kinyesi kiwe laini na kingi na huondoa kemikali
za sumu, na hivyo hufanya matumbo yawe na afya njema. Hupunguza uyeyushaji na
ufyonzaji wa virutubishi katika vyakula, na husaidia kupunguza unene.
 
Back
Top Bottom