Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuwalazimisha kushika imani kwa nguvu

Hakuna mzazi asiyependa mtoto wake awe mtu wa imani. Lakini tatizo linakuja juu ya ni kwa njia gani wazazi wanawawezesha watoto wao kushika imani.

Mzazi anapomlazimisha mtoto kushika imani, moja kwa moja mtoto ataiacha imani hiyo atakapokuwa mbali na mzazi; ni muhimu kumfanya mtoto atambue umuhimu wa imani yeye wenyewe na si kwa kumlazimisha. Hata hivyo unaweza kufanya haya yafuatayo kama mzazi:
 
Kuwa mfano wa kuigwa katika imani. Usimlazimishie imani ambayo wewe mwenyewe huna.
Mwonyeshe faida za kuishi kwenye imani.
Mwonyeshe athari za kuishi bila imani.
Mpe rasilimali zote zinazohitajika katika imani.
Fanyeni matendo ya kiimani pamoja katika familia (Kuomba, kusoma maandiko ya imani yenu, kujadili kwa pamoja maswala ya imani n.k.).
Mpongeze pale anapofanya jambo zuri la kiimani.
Kwa njia hii mtoto wako atakuwa katika misingi bora ya imani ambayo hataiacha.
 
Kutokuwa na muda wa kuwasikiliza

Wazazi wa leo kwa lugha ya mtaani wako “bize” kutafuta pesa na hawana muda na watoto. Ikumbukwe kuwa watoto nao wanahitaji kusikilizwa.

Mara kadhaa umewahi kusikia watoto waliojiua au kujidhuru kutokana na kuwa na matatizo ambayo walikosa mtu wa kumweleza. Hakikisha hata kama una shughuli nyingi kiasi gani hukosi muda wa kukaa na kumsikiliza mtoto wako.
 
Kugombana mbele ya watoto

Kuna wazazi wasiokuwa na staha kabisa, wao hutukanana na hata kupigana mbele ya watoto wao. Mtoto anapoona wazazi wakitukanana na kupigana, huiga tabia hiyo na kwenda kuifanya kwa wenzake na hata kwenye ndoa yake ya baadaye.

Ukiwa kama mzazi unayempenda mtoto wako, basi hakikisha tofauti zenu mnazimaliza kwa hekima na busara, tena ikibidi chumbani kwenu ili watoto wasipate mbegu mbaya kutoka kwenu.
 
Kuruhusu utamaduni wa kimagharibi uwatawale

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameingia mpaka kwenye swala la malezi. Wazazi wengi wa karne ya 21 wameruhusu watoto wao kutawaliwa na utamaduni wa kimagharibi.

Kwa mfano unamwekea mtoto televisheni yenye chaneli za kiasasa ua unamruhusu kutumia intaneti ya kawaida ambayo haijachujwa kwa ajili ya watoto. Ni wazi kuwa mtoto atajifunza tabia za ajabu ajabu kutoka kwenye tamaduni za kimagharibi zilizoporomoka.
 
Hata hivyo unaweza kufanya haya yafuatayo:

Usiruhusu mtoto wako kutumia televisheni au mtandao kwa muda mrefu.
Tawala chaneli na vipindi ambavyo mtoto wako anavitazama.
Tawala intaneti ya mtoto. Unaweza kumfungulia mtoto injini pekuzi (search engines)
 
Kuwa mkatili kwa mtoto

Naamini mara kadhaa umewahi kusikia mzazi amempiga mtoto hadi kufa au kumfanyia ukatili mwingine kwa kigezo tu kuwa mtoto amekosea.

Ni vizuri ukafahamu kuwa mtoto huonywa kwa hekima na upendo ili atambue kosa lake na afahamu kwanini ameadhibiwa ili asirudie kosa tena.

Kumfanyia mtoto ukatili kama vile kumchoma, kumkata, kumkanyagakanyaga, kumnyima chakula n.k. Humfanya akue katika hali ya kuwa mkatili au mwenye utu wa ndani ulioathirika.
 
Kumfanyia mtoto kila kitu

Wazazi wengi hufanya kosa la kumfanyia mtoto kila kitu kwa kuamini kuwa ndiko kumhudumia vyema. Watoto huwekewa wahudumu au waangalizi hata zaidi ya mmoja, ili tu wasipate shida.

Ni muhimu mtoto akajifunza kufanya baadhi ya vitu hata kama kuna mwangalizi; mtoto ajifunze vitu kama vile kuoga, kufua, kufagia na hata kupanga vitu katika chumba chake. Kwa njia hii utalea mtoto anayewajibika.
 
Kutokumfundisha mtoto kujiandaa kwa baadaye

Ni lazima mtoto afahamu kwanini anatakiwa kusoma, kulinda afya yake, kutumia pesa vizuri n.k. Wazazi wengi wanafikiri kuwa watoto watajua tu mambo haya wenyewe moja kwa moja siku za mbeleni.

Hili ni kosa ambalo huwafanya watoto wa wazazi wengi hasa wenye pesa kutokuandaa baadaye zao. Wao hufikiri wamezaliwa kutunzwa na baba na mama hadi mwisho wa maisha yao.
 
Kutokutawala ulaji wa mtoto

Ni jambo la kusikitisha kuona mtoto anapata maradhi ya shinikizo la damu kutokana na ulaji mbaya. Wazazi wengi wenye pesa huwapa watoto wao mlo bora kupita kiasi, jambo ambalo huathiri afya za watoto.

Pia wazazi wengine huwazoesha watoto wao vitu kama vile biskuti na pipi ili kuwafurahisha. Jambo hili limewasababishia watoto wengi kuoza meno au hata kuwa wezi wa fedha ili wanunue vitu hivyo.
 
Kutokumfundisha mtoto elimu ya jinsia

Swala la jinsia lipo na haliepukiki; mtu anayeweza kufahamu vyema maswala ya kijinsia ya mtoto ni mzazi. Watoto wengi hufundishwa elimu ya jinsia na marafiki zao shuleni, jambo linalowafanya wapate elimu potofu.

Hivyo ukiwa kama mzazi unayejali baadaye ya mtoto wako, ni vyema ukatenga muda ukazungumza naye kuhusu maswala ya kijinsia.
 
Kutokuheshimu hisia na utu wake

Mtoto ni binadamu kamili mwenye utu na hisia ambavyo vyote vinatakiwa kuheshimiwa. Wazazi wengi hufanya kosa la kutokujali kuwa watoto wao wamechoka, hawana furaha au hata kujali wanapokuwa na changamoto mbalimbali.

Ni muhimu pia wazazi waepuke kuwakaripia au kuwakemea watoto wao mbele ya watoto wengine, kwani kwa kufanya hivyo huwafanya wajisikie duni.
 
Back
Top Bottom