mzee wa liver
JF-Expert Member
- Dec 14, 2014
- 83,467
- 431,962
HahahahahaAaah!hata kama 6packs za bandia hazina mashiko bhana[emoji23][emoji23][emoji23]
Kutokuwa na muda wa kuwasikiliza
Wazazi wa leo kwa lugha ya mtaani wako “bize” kutafuta pesa na hawana muda na watoto. Ikumbukwe kuwa watoto nao wanahitaji kusikilizwa.
Mara kadhaa umewahi kusikia watoto waliojiua au kujidhuru kutokana na kuwa na matatizo ambayo walikosa mtu wa kumweleza. Hakikisha hata kama una shughuli nyingi kiasi gani hukosi muda wa kukaa na kumsikiliza mtoto wako.
We ujawahi kunywa mirinda nyeusi nini[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Wapenda mirinda nyeusi wewe[emoji23][emoji23][emoji23]
Ila novida tamu bhana
Kugombana mbele ya watoto
Kuna wazazi wasiokuwa na staha kabisa, wao hutukanana na hata kupigana mbele ya watoto wao. Mtoto anapoona wazazi wakitukanana na kupigana, huiga tabia hiyo na kwenda kuifanya kwa wenzake na hata kwenye ndoa yake ya baadaye.
Ukiwa kama mzazi unayempenda mtoto wako, basi hakikisha tofauti zenu mnazimaliza kwa hekima na busara, tena ikibidi chumbani kwenu ili watoto wasipate mbegu mbaya kutoka kwenu.
Kutokuheshimu hisia na utu wake
Mtoto ni binadamu kamili mwenye utu na hisia ambavyo vyote vinatakiwa kuheshimiwa. Wazazi wengi hufanya kosa la kutokujali kuwa watoto wao wamechoka, hawana furaha au hata kujali wanapokuwa na changamoto mbalimbali.
Ni muhimu pia wazazi waepuke kuwakaripia au kuwakemea watoto wao mbele ya watoto wengine, kwani kwa kufanya hivyo huwafanya wajisikie duni.
Kutokumfundisha mtoto elimu ya jinsia
Swala la jinsia lipo na haliepukiki; mtu anayeweza kufahamu vyema maswala ya kijinsia ya mtoto ni mzazi. Watoto wengi hufundishwa elimu ya jinsia na marafiki zao shuleni, jambo linalowafanya wapate elimu potofu.
Hivyo ukiwa kama mzazi unayejali baadaye ya mtoto wako, ni vyema ukatenga muda ukazungumza naye kuhusu maswala ya kijinsia.