MFALME. Mfalme alitafuta maji safi ya kunywa asiyaone. baada kutembea sana na uchovu na kiu, akayakuta maji yasiyo safi wala salama, akayarukia na kuyabugia. Kwa uchovu, kiu na njaa aliyokuwa nayo, siku hii ya pili mfalme hakutembea sana. Akaamua ajipumzishe hapo karibu na maji maana ilionekana kwamba maji kwenye pori hilo ni changamoto kubwa. hivyo, mchana ule uliobakia mfalme akaamua kutafua kieneo hapo akauchapa usingizi. Alipoamka ni jioni, akatafuta mti, akaupanda kuyapisha matukio ya usiku. Kesho yake mfalme akaanza kuona hali halisi ya hatari ya yeye kuwa mpori pori. maana jitihada zake za kuona angalau dalili ya binadamu hazikuwapo. Akajipa moyo akaanza tena kuchapa mwendo, alipiga mwendo asimuone hata mwanadamu wala dalili za kuona mtu, akazidi kuteseka kimwili na kifikra lakini hakuwa na namna
INAENDELEA....