Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Matangazo yanayokera

Nani asiyependa kupata pesa kupitia blog? Naamini hakuna; ikiwa unapenda kuweka matangazo mbalimbali kwenye tovuti au blog yako hakikisha matangazo husika hayamkeri mtumiaji.
 
BZxDAnlh2I4.jpg
 
Kukosekana kwa kurasa za msingi

Kuna kurasa za msingi zinazopaswa kuwepo kwenye kila tovuti (website) au blog; kurasa hizo ni kama vile: Kutuhusu, Wasiliana nasi, Sera ya faragha, Vigezo na masharti n.k.

Kurasa hizi zitamwezesha mtumiaji kufahamu kuhusu tovuti au blog pamoja na wamiliki wake; pia zitamwezesha mtembeleaji kufahamu njia za kupata msaada au kuwasiliana na wahusika.
 
Si hayo tu, bali hata sheria na kanuni zinazotawala tovuti husika zitaonekana vyema kwenye kurasa hizi.

Hivyo ni muhimu kuhakikisha hupuuzi nafasi ya kurasa hizi. Kumbuka! Google hawawezi kutangaza kwenye tovuti au blog ambazo hazina kurasa hizi.
 
Kumuunganisha mtembeleaji bila ridhaa yake

Unahitaji watembeleaji wajiunge kwenye orodha yako ya barua pepe au vitaarifu? Kama jibu ni ndiyo, basi usiwaunge kwa lazima kwani wataichukulia tovuti au blog yako kuwa inaingilia uhuru wao binafsi.

Hakikisha umempa mtembeleaji kitu chenye manufaa kitakachomfanya aone kuwa kuna umuhimu wakujiunga kwenye tovuti au blog yako.
 
Kukusanya taarifa za mtumiaji kwa siri

Kukusanya taarifa za mtumiaji kwa siri bila ridhaa yake ni kosa kisheria; ni lazima ufahamu sera na taratibu zinazotawala faragha ya mtumiaji.

Hivyo kuwa makini unapotaka kukusanya taarifa kama vile jina, barua pepe, umri, jinsia, aina ya kifaa alichotumia, anwani mtandao n.k. Hakikisha mtumiaji wa tovuti au blog yako anafahamu wazi aina ya taarifa unazokusanya pamoja na matumizi yake.
 
Uandishi duni

Uandishi wa kwenye tovuti siyo sawa na ule wa kwenye kitabu au andiko la chuo kikuu. Hivyo ni muhimu ukajifunza uandishi bora na rafiki kwa wasomaji pamoja na injini pekuzi (search engines). Unaweza kuhakikisha haya yafuatayo:
 
Kosa la kutumia viunganishi vilivyojificha

Inawezekana unataka kuweka kiunganishi mahali ambapo mtembeleaji wa tovuti au blog yako atakibonyeza bila yeye kujua; jambo hili ni baya kwani linakiuka kanuni za kuheshimu matakwa ya watembeleaji.

Hakikisha hufanyi kosa hili kwani hata injini pekuzi kama Google zinasisitiza kuepuka swala la kuficha viunganishi.
 
Kutozingatia kanuni za uboreshaji wa injini pekuzi (Search Engine Optimization -SEO)

Watu wengi wanaanzisha tu blog na tovuti bila kujifunza wala kufahamu umuhimu wa uboreshaji wa injini pekuzi. Uboreshaji wa injini pekuzi ni muhimu kwani utafanya tovuti au blogu yako ionekane kwa watembeleaji. Hivyo hakikisha unafanya uboreshaji wa injini pekuzi jinsi ipasavyo. Unaweza kuzingatia haya:
 
Chagua mada nzuri ya kuandika.
Epuka kunakili makala ua maudhui kutoka kwenye blog au tovuti nyingine.
Andika kwa uandishi mzuri ambao unasomeka bila shida.
Tumia picha vizuri.
Andika makala au chapisho lenye urefu wa kutosha.
Weka taarifa za meta kwenye kila ukurasa (Maelezo ya ukurasa pamoja na kichwa.) Ikiwa unatumia WordPress unaweza kutumia Yoast SEO itakusaidia sana.
 
Matumizi ya maandishi yanayochezacheza

Maandishi yanayochezacheza (blink) yamepitwa na wakati toka miaka ya 1990, hivyo kutumia maandishi haya hakumsaidii mtumiaji kwa njia yoyote bali humfanya aone tovuti yako ni ya kizamani. Kumbuka kuwa vivinjari mbalimbali havitambui tena mfumo wa maandishi haya.
 
Matumizi makubwa ya teknolojia ya flash

Flash ni teknolojia ya kuweka video, picha, na sauti kwenye tovuti. Kwa kiasi kikubwa ina changamoto nyingi na imeshapitwa na wakati.

Matumizi ya teknolojia ya flash hufanya tovuti ifunguke kwa shida pamoja na kumuweka mtumiaji katika hatari ya kudukuliwa na wadukuzi wanaolenga teknolojia hii.

Inashauriwa kuepuka kosa hili la kutumia flash na badala yake utumie teknolojia ya HTML5
 
Mfumo duni wa viunganishi (menu and navigation)

Mfumo wa viunganishi (menu) ni muhimu sana kwenye tovuti yako, hivi humwezesha mtumiaji kuhama kutoka eneo moja la tovuti au blog yako hadi lingine.

Ni vyema ukahakikisha mpangilio na mfumo wa viunganishi katika tovuti yako umekaa vizuri na unaeleweka.
 
Back
Top Bottom