Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SAMBUSA ZA NYAMA MAHITAJI manda za sambusa Unga wa ngano 1/4kilo Maji kiasi Chumvi kiasi Sukari kidogo Mafuta Mchanganyiko wa kuweka 1/4 kilo nyama ya kusaga 3 vitunguu maji 1 karoti kubwa 1 pilipili hoho 1tsp tangawizi na kitunguu saumu Giligilani ,beef masala,pilipili manga,chumvi kiasi Mafuta ya kupikia km lita 1 Njia Njinsi ya kutengeneza manda Changanya unga,maji,chumvi,sukari na mafuta kidogo kanda mpk upate donge laini la wastani kisha katakata donge dogodogo na chukuwa anza kuweka shape ya chapati kisha paka mafuta na weka jingi juu na paka mafuta mpk umalize yote kisha sukuma chapati moja kubwa na choma kwy frypan pande zote kisha kata mara nne na utenganisha na uziweke kwy kitambaa au friji ili zisikauke Jinsi ya kutengeneza mchanganyiko Anza kuweka nyama acha kidogo maji yaishe kisha weka vitunguu maji,vitunguu saumu ,tangawizi ,karoti ,pilipili hoho,chumvi ,beef masala,pilipili manga ,giligilani na mafuta kiasi kisha changanya acha mpk iive . Epua na acha ipowe na kisha chukuwa manda zako na anza kuzifunga kwa kuweka nyama zako ndano ma pale pa kufungia paka uji mzito wenye unga na maji ili kufunga Choma kwy mafuta yaliyopata moto kwa ile rangi ya kahawia. Manda zilizobaki unazichoma pia kwy mafuta kupata kaukau usizitupe . Tayari kwa kuliwa.
 
GRILLED CHICKEN MAHITAJI Kuku 1/2 (mkate vipande vikubwa) Tangawizi 1/2 tsp Kitunguu saum 1/2 tsp Chumvi kiasi Limau (lemon juice) 1tbsp Sweet chilli sauce 2 tbls Pilipili manga 1/2 tsp Mafuta 2tbsp Kitunguu maji 1/2 (sliced) JINSI YA KUTENGENEZA Mchanganye kuku na vitu vyote kasoro vitunguu Muache kwa muda akolee viungo mchome kwa grill pande zote akianza kupiga rangi tia vitunguu wacha viwive na kuku mpaka akipiga rangi vizuri mtowe Enjoy
 
NDIZI ZA KUKAANGA (PLANTAINS) MAHITAJI ndizi mbizu (ripe plantains) 3 Mafuta ya kupikia (cooking oil) 5 tblsp Chumvi kidogo (pinch of salt) MATAYARISHO zikoshe ndizi na maganda yake kisha zikate size unopenda (zikate na maganda yake ndio zinakatika vizuri). Ukimaliza kuzikata ndio unazimenya, ziweke kwenye bakuli weka chumvi mix kidogo. Weka frying pan kwenye jiko, tia mafuta ukiona kidogo ongeza lakini yasiwe mengi yakafunika ndizi wakati wa kukaanga. Zikaange pande zote mbili usiziache sana zinaiva mara moja. ENJOY ni tamu sana.
 
Liverpool na Manchester United zitakutana tena Jumamosi Mashetani Wekundu wa Jose Mourinho watakapozuru Anfield
Pointi saba tayari zinazitenganisha timu hizo mbili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza, lakini hii mechi hii itakuwa mtihani wa uwezo wa Manchester United na Liverpool katika harakati zao kwenye mbio ubingwa.
Manchester United hawajashinda mechi nne za mwisho dhidi ya Liverpool katika michuano yote, ingawa mechi tatu za mwisho baina ya timu hizi maarufu ziliishia sare.
 
Mechi kama hii msimu uliopita ilikuwa sare tasa katika uwanja wa Anfield.
Liverpool wameshindwa kuifunga United katika mechi sita za mwisho Ligi Kuu, mara ya mwisho walishinda Septemba 2013 katika uwanja wa Anfield, Daniel Sturridge alipofunga goli pekee la mechi hiyo.
Danny Murphy anaamini mechi hii ya Jumamosi itakuwa ni kubwa kwa Liverpool kuliko kwa Manchester United kwani United tayari wameshavuna pointi nyingi na mwenendo wao ni mzuri.
 
Liverpool ni timu ambayo imekuwa ikipewa nafasi kubwa katika mbio za ubingwa baada ya kushinda 4-0 dhidi ya Arsenal, lakini imekuwa ni habari tofauti kwa sasa.
Wameshinda mechi moja tu kati ya saba baina ya mapumziko ya kimataifa, Reds sasa wanashika nafasi ya saba kwenye jedwali la Ligi Kuu, bila ya ushindi kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa na wameshatolewa kwenye michuano ya Kombe la EFL kufuatia mwenendo mbaya Septemba.
 
Pengo baina yake na klabu za Manchester zinazoshikilia usukuni tayari ni pointi saba, na ikiwa itakubali kichapo Jumamosi basi pengo litaongezeka hadi 10. Ikiwa bado ni mapema sana kusema chochote kuhusu jedwali la ligi, deni la pointi 10 litakuwa mzigo mkubwa kwa Liverpool kuzifukuzia City na United ambazo zitakuwa mbali sana.
Kusema mechi hii ni lazima ushindi haitakuwa haki kwa Liverpool - wamepoteza mechi moja Ligi Kuu msimu huu na wanapungukiwa pointi moja tu kutoka timu inayoshika nafasi ya nne.
 
Mfumo wa Jurgen Klopp hauruhusu timu kufungwa kirahisi, ingawa kushinda pia si rahisi, Mjerumani huyo huenda asibadili falsafa yake dhidi ya United wikiendi hii.
Safu ya ulinzi imekwa tatizo la muda mrefu, na Klopp amekiri kuwa anachoshwa na tatizo hilo, lakini tatizo jingine kwa Liverpool ni kupoteza nafasi nyingi mbele ya goli. Pointi nyingi walizopoteza ni katika mechi walizomiliki mchezo kwa kiasi kikubwa lakini hawakufanikiwa kuziona nyavu.
 
Sare dhidi ya Burnley na Leicester City - na mapema msimu huu dhidi ya Watford - Liverpool hawana jipya lakini watapambana kuweka rekodi dhidi ya mahasimu wao.
United imekuwa tofauti msimu huu, na Liverpool hawajashinda tangu Agosti, Iwapo Mashetani Wekundu watacheza kwa kushambulia zaidi hali itakuwa mbaya kwa Vijogoo wa Anfield.
 
Kufuatia mwenendo mbaya msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Uingereza, Manchester United ya Mourinho sasa inafidia muda waliopoteza na wanawapa presha mahasimu wao Man City.

Wakiwa wamepoteza pointi 23 msimu uliopita, United wameanza kampeni hizi kwa rekodi nzuri mbele ya mashabiki wao, na mechi zao za ugenini wamekuwa wakifanya vizuri wakiwa wamepata sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City, mechi pekee waliyotetereka.
 
Kufuatia mwenendo mbaya msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Uingereza, Manchester United ya Mourinho sasa inafidia muda waliopoteza na wanawapa presha mahasimu wao Man City.

Wakiwa wamepoteza pointi 23 msimu uliopita, United wameanza kampeni hizi kwa rekodi nzuri mbele ya mashabiki wao, na mechi zao za ugenini wamekuwa wakifanya vizuri wakiwa wamepata sare ya 2-2 dhidi ya Stoke City, mechi pekee waliyotetereka.
 
Maswali bado yapo juu ya uwezo wao kuwania taji, City wameshajitwalia pointi nyingi katika mechi dhidi ya Chelsea na Liverpool, mechi ya wikiendi hii itakuwa jaribio kubwa kwa United kwani watakutana na moja ya mahasimu wao sita wakuu.
Ni kweli kwamba, timu ya Mourinho husambaratisha kila wanayekutana naye na mwendo wa mechi 10 bila kufungwa ni pamoja na mechi tisa walizoshinda, haijalishi walikutana na mpinzania gani, lakini mechi hii ya Anfield ndio mtihani wao wa Jumamosi.
 
United ina wastani wa magoli matatu kwa mechi katika Ligi Kuu Uingereza msimu huu na wapo nyuma ya Man City kwenye chati ya magoli, wamefunga mabao manne kwa mechi katika mechi sita.
United wana kikosi bora zaidi kuikabili Liverpool zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita, lakini Mourinho atalazimika kuwa mkali zaidi ili kuhakikisha wanashinda na kuwaongezea presha Man City.
 
Liverpool imepata pigo baada ya winga wao Sadio Mane kupata majera mara baada ya kumaliza adhabu yake - na kuna uwezekano mkubwa akakaa nje wiki sita kuuguza majeraha aliyopata kwenye jukumu la kimataifa akiwa na Senegal.

Hapakuwa na matatizo makubwa ya majeruhi kipindi cha mapumziko ya kimataifa, ingwa Philippe Coutinho na Georgenio Wjnaldum walifanya mazoezi tofauti na kikosi cha Liverpool Alhamisi.
Dejan Lovren alitolewa kwenye mechi ya Croatia kufuzu dhidi ya Finland lakini alicheza wakishinda dhidi ya Ukraine na anatarajiwa kuwa fiti wikiendi hii licha ya kukiri kuwa naishi kwa dawa za kupunguza maumivu kabla ya mechi zote.
Nathaniel Clyne na Adam Lallana bado wataendelea kukosekana kwenye kikosi cha Reds, Alex Oxlade-Chamberlain anaweza kuanza mechi ya kwanza Ligi Kuu akiwa na klabu hiyo.
Manchester United wamepata pigo katika mapumziko ya mapumziko ya kimataifa baada ya Marouane Fellaini kupata majeraha ya ligamenti akiwa Ubelgiji, jambo litakalompa Mourinho maumivu ya kichwa kwani Paul Pogba na Michael Carrick hawapo pia.
Kikosi tarajiwa Liverpool:
Mignolet; Alexander-Arnold; Matip, Lovren, Moreno; Oxlade-Chamberlain, Henderson, Can; Salah, Firmino, Coutinho
Kikosi tarajiwa Man Utd:
De Gea; Valencia, Bailly, Jones, Young; Matic, Herrera, Mata, Mkhitaryan, Rashford; Lukaku
 
a5d10ef64c7dfff5527a6e06ed425c5a.jpg
 
Back
Top Bottom