Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

df721ef405cd6dee9be5f186c828c55e.jpg
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Hulali jamani,Jaribu kulala pls
OK baby. Uwe na siku njema...[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji25][emoji25][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
OK baby. Uwe na siku njema...[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji124]‍♂️[emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji42][emoji25][emoji25][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
Asantee love[emoji9] [emoji9] [emoji9]

Lala salama,Malaika wa Mungu wakulinde.
 
Kuku mzima (makange style) Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu nusu kijiko Tangawizi nusu kijiko Curry powder nusu kijiko Masala nusu kijiko Limao Nyanya 3 Karoti 1 Kitunguu maji 1 Pilipili hoho nusu Chumvi Mafuta Njia Pasua kuku katikati kisha mpake limao na chumvi na kisha acha nusu saa na kisha mkaange kuku mzima kwy mafuta mpk aive awe rangi ya kahawia Kisha pembeni anza kwa kuweka mafuta kidogo kwy sufuria kisha weka kitunguu maji acha iwe na rangi ya kahawia kisha weka kitunguu saumu tangawizi curry powder na masala na kaanga kisha weka karoti pilipili hoho na endelea kukaanga kisha weka chumvi na ikisha ivaa mweke kuku wako kwy huu mchanganyiko aingii pande zote za kuku na kisha epua Kula na chochote ukipendacho ugali wali chips
 
PILAU YA NYAMA YA KUSAGA MAHITAJI mchele vikombe 2 Nyama ya ngombe ya kusaga 1/4 kilo Njegere kiasi Kitunguu maji 3 Kitunguu saumu kijiko 1 cha chai Tangawizi nusu kijiko Pilau masala kijiko kimoja Curry powder 1/2 kijiko Royco 1/2kijiko Beef masala1/2 kijiko Mafuta ya kupikia na chumvi Kachumbari Kitunguu maji 1 Nyanya 2 Tango nusu Limao 1/2 Pilipili 1 Njia Weka mafuta kiasi jikoni kisha weka vitunguu subiri vianze kubadili rangi kisha weka kitunguu saumu na tangawizi baada ya hapo weka njegere ulizozichemsha pembeni na nyama acha kwa muda kidogo kisha weka viungo wako pilau masala,curry powder,royco,beef masala na chumvi kisha acha viungo viingii vizuri kwy nyama ya kusaga na viive kisha weka mchele wako na ongeza maji ya moto kiasi kulingana na mchele wako funika na acha mpk pilau likaukii kw moto wa wastani Kachumbari Katakata vitunguu osha na chumvi na maji kiasi kuondoa ukali kisha katia nyanya na tango kwa style yote upendayo kisha weka chumvi,pilipili na limao changanya tayari kwa kuweka kwenye pilau letu Kwa wapenzi wa mayonase unaweza ukaongeza
 
DAGAA WA NAZI NA MAZIWA Mahitaji Dagaa wa mwanza robo kilo Kitunguu maji 1 Nyanya 3 Pilipili hoho nusu Karoti 1 Tui la nazi zito 1/2kikombe Maziwa fresh 1/2 kikombe Kitunguu saumu na tangawizi1/4kijiko cha chai Royco 1 kijiko Beef masala 1 kijiko Binzari ya manjano1/4kijiko Mafuta kiasi Chumvi kiasi Njia Chukuwa sufuria weka mafuta subiri yachemke kisha weka kitunguu kaanga kidogo kisha weka vitunguu saumu na tangawizi endelea kukaanga upate rangi ya kahawia kisha weka karoti pilipili hoho na nyanya endelea kukaanga kisha weka dagaa zako na weka maji au tui la pili km umetumia nazi ya kawaida kisha weka dagaa zako Baada ya hapo weka viungo wako royco binzari na beef masala na chumvi na ongeza maji au tui la pili funika acha ive kwa muda ukishaona imeiva weka tui lako na maziwa acha kwa muda kidogo. Epua na tayari kwa kuliwa haswa na ugali Enjoy -
 
Nyama ya mbuzi choma (simple) Mahitaji Nyama ya mbuzi kilo moja Kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai Tangawizi kijiko kimoja cha chai Limao moja Chumvi Mafuta vijiko viwili Njia Chukua nyama yako weka viungo vyote kitunguu saumu, tangawizi limao,chumvi na mafuta na unahakikisha viungo vyako vinaingia vizuri kwy nyama Kisha weka funika na weka kwy friji kwa masaa 7 au usiku mzima ili viungo vyako viingii vizuri kwy nyama Kisha bake 160°c kwa masaa 2 au unaweza kuchoma kwy jiko la mkaa lenye wavu juu kwa masaa mawili hakikisha moto ni mdogo ili aive vizuri. Tayari kwa kula
 
Kuku wa kuchoma Mahitaji Kuku mzima Kitunguu saumu 1 tsp Tangawizi 1 tsp Limao Binzari ya manjano 1/2 tsp Garam masala 1/2 tsp Curry powder 1/2 tsp Chumvi Mafuta vijiko 2 Njia Chukuwa kuku muweke mahitaji yote kitunguu saumu, tangawizi,limao,binzari ya manjano,garam masala,curry powder,chumvi na mafuta na mpake hakikisha anaingia vizuri kwy kuku na kisha muweke kwy friji chini kwa muda wa saa 6 au hata usiku mzima Kisha washa oven 200°c na muweke kuku wako kwa muda wa saa 1 kisha mpasue katika ili kumfungua ili achomeeke vizuri kwa ndani kwa muda wa dk 35 na tayari na hakikisha anapata yangi nzuri ya kahawia. Enjoy unaweza kula na chochote ni mtamu sana
 
POUND CAKE mahitaji Unga wa ngano vikombe 2 Sukari kikombe 1 Siagi kikombe 1 Mayai 5 Vanilla extract 2 tsp Maziwa ya maji vijiko 4 Baking powder 1 1/2 tsp Njia 1. Chukuwa chombo changanya unga wa ngano na baking powder na uchekeche unga wako mara 2 mpk 4 hii inasaidi keki kuwa laini 2.chukuwa siagi kisha weka sukari na anza kusaga kwa kutumia mashine au mwiko mpk ilainike kabisa na anza kuweka yai moja baada ya jingine huku unaendelea kuchanganya mpk umalize yote na mchanganyiko utakuwa laini malizia kwa kuweka vannila na saga ili ichanganyike vizuri 3.kisha chukuwa ule unga wako na changanya na mchanganyiko wako na weka yale maziwa koroga ichanganyike vizuri 4.chukuwa chombo cha kubake paka siagi na unga wa ngano na kisha weka mchanganyiko wako na bake kwy oveni 200°c kwa dakika 45 kisha angalia km tayari kwa kuweka toothpick katika ikitoka safi keki tayari 5.subiri ipoe na tayari kwa kuliwa au unaweza pamba upendavyo
 
MOROCCAN CHICKEN EGGPLANT AND TOMATOES STEW MAHITAJI 3 vijiko vya mafuta ya kupikia kuku 1 mzima wa kisasa Kitunguu maji 1 Biringanya 4 Nyanya kubwa 5 Maji vikombe 2 1/2 Binzari nyembamba tsp 1 Binzari ya manjano tsp 1 Kitunguu saumu tsp 1 Tangawizi tsp1 Paprika 1 tsp Limao 1 Chumvi kiasi Pilipili manga kiasi NJIA Chukuwa sufuria ya kupikia weka mafuta kisha weka kuku wako na koroga huku unamgeuza kuku akauke maji na anze kupata rangi ya kahawia kisha weka vitunguu ,biringanya na nyanya ulizokataka na acha km dakika 5 na baada ya hapo weka vitunguu saumu, tangawizi,paprika,binzari ya manjano na nyembamba ,chumvi na pilipili manga na koroga mpk ichanganyike vizuri. Kisha kamulia limao na weka maji funika na acha mpk kuku aive na maji ya pungue . Epua na tayari kwa kuliwa na chochote utakachopenda kama wali,ugali,viazi,mihogo,mkate nk.
 
Back
Top Bottom