Liverpool imepata pigo baada ya winga wao Sadio Mane kupata majera mara baada ya kumaliza adhabu yake - na kuna uwezekano mkubwa akakaa nje wiki sita kuuguza majeraha aliyopata kwenye jukumu la kimataifa akiwa na Senegal.
Hapakuwa na matatizo makubwa ya majeruhi kipindi cha mapumziko ya kimataifa, ingwa Philippe Coutinho na Georgenio Wjnaldum walifanya mazoezi tofauti na kikosi cha Liverpool Alhamisi.
Dejan Lovren alitolewa kwenye mechi ya Croatia kufuzu dhidi ya Finland lakini alicheza wakishinda dhidi ya Ukraine na anatarajiwa kuwa fiti wikiendi hii licha ya kukiri kuwa naishi kwa dawa za kupunguza maumivu kabla ya mechi zote.
Nathaniel Clyne na Adam Lallana bado wataendelea kukosekana kwenye kikosi cha Reds, Alex Oxlade-Chamberlain anaweza kuanza mechi ya kwanza Ligi Kuu akiwa na klabu hiyo.
Manchester United wamepata pigo katika mapumziko ya mapumziko ya kimataifa baada ya Marouane Fellaini kupata majeraha ya ligamenti akiwa Ubelgiji, jambo litakalompa Mourinho maumivu ya kichwa kwani Paul Pogba na Michael Carrick hawapo pia.
Kikosi tarajiwa Liverpool:
Mignolet; Alexander-Arnold; Matip, Lovren, Moreno; Oxlade-Chamberlain, Henderson, Can; Salah, Firmino, Coutinho
Kikosi tarajiwa Man Utd:
De Gea; Valencia, Bailly, Jones, Young; Matic, Herrera, Mata, Mkhitaryan, Rashford; Lukaku