Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

double
 
Ni kweli Kiongozi.

Robert sio Mtu mzuri hata kidogo.

Na alikuwa na mpango wa kumuoa.

Ingawa kulikuwa na Uvumi wa kichini chini ya kuwa walishafanya Ndoa ya Siri
Aisee. Jamaa naye huwa haangalii makunyanzi. Ile kesi nyingine aliyokuwa akishtakiwa kwa kulala na kasichana kengine under age na wakajirekodi kabisa naona alichomoa. Inaonekana jamaa ni hatari sana !!!
 
Okwi ameendeleza ufalme wake uwanja wa Uhuru baada ya kufunga bao lake la saba kwenye uwanja huo alipoinusuru Simba dhidi ya Mtibwa Sugar
Goli la Emmanuel Aronld Okwi dakika ya 90 na sekunde kadhaa limeinusuru Simba kulala mbele ya Mtibwa Sugar baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Shakaile Shangalai kutoka Pwani, aliyesaidiwa na Janet Balama wa Iringa na Sylvester Mwanga wa Kilimanjaro, hadi mapumziko Mtibwa Sugar walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Simba ikicheza dhidi ya Mtibwa Sugar, iliruhusu bao la mapema dakika ya 36 lililofungwa na Stamili Mbonde kwa kichwa kikali.
 
Pamoja na kuondoka uwanjani wako nyuma kwa bao 1-0, lakini ni Simba waliocheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Mtibwa Sugar, ingawa tu wakashindwa kutumia nafasi.
Kipindi cha pili, kocha Mkameruni, Joseph Marius Omog alikianza kwa kufanya mabadiliko katika safu yake ya ulinzi, akimtoa beki Salim Mbonde aliyeumia na kumuingiza Mganda, Juuko Murshid.
 
Hata hivyo, Mtibwa Sugar wakaendelea kung’ara uwanjani na dakika ya 51 Mbonde akapoteza nafasi ya wazi ya kufunga tena baada ya pasi nzuri ya Salum Khamis, akapiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa Aishi Manula.
Mtibwa Sugar ilipata pigo dakika ya 57, baada ya Mbonde kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake anaingia Kelvin Sabato Kongwe.
 
Kipa Benedictor Tinocco wa Mtibwa akaokoa shuti la Okwi aliyepokea pasi nzuri ya Jonas Mkude dakika ya 61 na dakika ya 72 kiungo Hassan Dilunga naye akapiga shuti dhaifu baada ya pasi nzuri ya Kelvin Sabato likaishia mikononi mwa Manula.
Dakika ya 90 na masekunde, beki Cassian Ponera akamvuta beki wa Simba nje kidogo ya boksi na refa Shakaile Shangalai akatenga mpira wa adhabu ambao Okwi alikwenda kupiga kiufundi na kuisawazishia Simba.
 
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Tanzania aliiwezesha timu yake Genk kupata pointi moja kwa kutoa pasi ya bao la kusawazisha dhidi ya Royal Excel
Mbwana Samatta alikuwa kwenye kikosi cha kwanza na alicheza dakika zote 90 katika mechi ya Jumamosi KRC Genk ikiendelea kupita katika kipindi kigumu mwanzo wa msimu huu baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Royal katika uwanja wa nyumbani.
 
Vijana wa Albert Stuivenberg walionyesha kandanda safi dhidi jitihada za timu ya Mircea Rednic na walihakikisha hawapotezi pointi zote tatu, shukrani kwa bao la kusawazisha la Marcus Ingvartsen.
Royal Excel Mouscron walipata goli la kuongoza mnamo dakika ya 42 Dorin Rotariu akifunga kwa guu lake la kulia akiunganisha pasi ya Sebastien Locigno, kupeleka shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo ya ugenini.
 
Mtanzania, Samatta hakuwa na bahati ya kufunga, lakini alikimbia mara zote na mpira, bila ushindani mwingi sana lakini bahati haikuwa upande wake.
Marcus Ingvartsen hakufanya makosa zikiwa zimebakia dakika tisa mechi kumalizika, alifunga akiunganisha pasi matata ya Samatta na kumshinda kipa Logan Bailly kusawazisha dakika ya 81 ya mchezo.
 
Hiyo ni mechi ya 66 kwa Samatta akiwa na Genk kwenye michuano yote tangu Januari 2016 alipojiunga na klabu hiyo akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Samatta aliyekuwa mchezaji bora wa Africa wa Mwaka 2016 amecheza mechi yake ya 66, 38 akianzia kikosi cha kwanza na 24 akitokea benchi.
 
Back
Top Bottom