Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

madhara ya fistula ni yapi?
kibovu cha mkojo kuondoka sehemu yake
kupata ugonjwa wa njia ya mkojo mara kwa mara
ugumba
kuishiwa damu
sehemu za uke wa mwanamke kuharibika
kuvunjika kwa ndoa
kutengwa na jamii
kujiua kwa wahanga wa tatizo hili.
[emoji256][emoji256]jinsi gani tunaweza kuzui fistula kwenye jamii zetu?
kuzuia wasichana wadogo kuzaa
hakikisha mama hakai na uchungu zaidi ya masaa 12 baada ya uchungu kuanza
hakikisha mama anazalia hospitali ili asaidiwe vizuri
kuweka miondominu mizuri kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa.
 
VIPIMO VYA KUPIMA KIPINDI CHA UJAUZITO

watu wengi hua wakipata ujauzito hukaa na mimba zao nyumbani huku wakidi wanasubirii zikue kidogo halafu waende kliniki kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. kikawaida ukigundua tu una mimba hata kama ina wiki moja au mbili nenda kliniki ambapo utapimwa vipimo kadhaa muhimu ambavyo ni muhimu sana kwa ujauzito wako na lakini pia kuna baadhi ya magonjwa yasipogundulika basi yatasababisha mimba kutoka, mtoto kuzaliwa kabla ya muda, kuzaliwa mfu au kuzaliwa akiwa akiwa hana akili nzuri. hata kama ukiambiwa vipimo hivi havipo basi jitahidi ukavitafute hata hospitali binafsi kwa usalama wako.vipimo hivyo ni kama vifuatavyo.
 
wingi wa damu; h ichi ni moja ya vipimo muhimu sana kwa wajawazito kwani upungufu wa damu kipindi hiki ni moja ya vyanzo vikuu vya kifo cha mama na mtoto.jipindi hiki mama damu yake haitakiwi ipungue chini ya 10g/dl na hutakiwa kutumia virutubisho vya kuongeza damu kama madini ya chuma, folic acid au mchanganyiko wa vyote kwa jina la haemovit.
 
virusi vya ukimwi; kuna watu wengi ambao ni waathirika wa virusi vya ukimwi lakini hawajui, kipindi hichi ni muhimu sana kujua afya wako kwani mimba inapunguza sana kinga ya mwili na kutafuna virutubisho kwenye mwili wa mama ili mtoto akue. hivyo ikifahamika wewe ni muathirika utapata faida kuu mbili; kwanza kupewa dawa za kuzuia maambukizi ya mtoto aliyeko tumboni na wewe pia kuishi vizuri pili uweze kuwalinda uwapendao.
 
kipimo cha malaria : unaweza kua unadharau huu ugonjwa lakini ni moja ya vyanzo vikuu vya kutoka mimba, ndio maana mama hupewa vidonge vya sp katika kipindi fulani cha ujauzito ili kujizuia na malaria. lakini pia malaria inawez a kuua mama na mtoto hivyo kutumia neti kipindi hki ni muhimu sana.
 
vipimo vya magonjwa ya zinaa; ugonjwa wa kaswende ni mmoja wa magonjwa hatari sana, dalili zake zinaweza zisiwe rahisi kujua lakini hutoa mimba sana. hivyo ni vizuri kupima kaswende na magonjwa mengine ya zinaa kama gonorea na herpes simplex virus ambayo huweza kuleta upofu kabisa kwa mtoto.
 
kipimo cha choo ndogo na kubwa; choo ndogo hupimwa ili kuangalia kama hakuna ugonjwa wowote wa njia ya mkojo kwani ugonjwa wa uti huweza kuleta uchungu na kutoa mimba lakini pia huwasumbua sana akina mama kipindi cha ujauzito. choo kubwa mara nyingi hupimwa kuangalia minyoo.baadhi ya minyoo hutumia damu kama chakula na inaweza kusababisha upungufu mkubwa wa damu mwilini.mfano hook worms..
 
mwisho; kuna maelekezo mengi na mahudhurio kadhaa mabayo mama hutakiwa ayafanye mpaka kipindi cha kujifungua, hivyo ni vema kwenda kliniki kama ulivyoelekezwa na kupokea chanjo zote muhimu na virutubisho muhimu ili kumpata mtoto mzima na mwenye afya.
 
Yajue magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kwa watoto

Makala haya yanachambua maandiko mbalimbali toka Mpango wa Taifa wa Chanjo ulioanzishwa ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo katika maisha ya mtoto. Nchini Tanzania magonjwa yanayokingwa kupitia kwa chanjo ni polio, kifua kikuu, pepopunda, dondakoo, kifaduro, homa ya ini, homa ya uti wa mgongo, surua, nimonia na rotavirus. Huduma za chanjo ni mkakati muafaka katika kutokomeza maradhi tajwa hapo juu na kupunguza vifo vya watoto na akina mama nchini Tanzania. Hivyo basi chanjo ni muhimu katika uhai na maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla. Kila mzazi/mlezi hana budi kuhakikisha mtoto anapatiwa chanjo zote ili kumkinga na magonjwa yanayokingwa kwa chanjo.
 
Kifua kikuu
ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bakteria na huenezwa kwa njia ya hewa. Mtu mwenye maambukizi ya kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hivyo hewani na huweza kumwambukiza mtu mwingine. Ugonjwa huu unakingwa kwa chanjo ya kifua kikuu (BCG), ambayo hutolewa mara tu mtoto anapozaliwa au anapofika kliniki kwa mara ya kwanza. Iwapo kovu halitajitokeza chanjo irudiwe katika kipindi cha miezi 3. Mzazi au mlezi hakikisha kila mtoto anapozaliwa anapata chanjo ya kuzuia kifua kikuu kwani itamkinga dhidi ya ugonjwa huu.
 
Ugonjwa wa polio
husababishwa na virusi vya polio, ambavyo huenezwa kwa njia ya kula na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi. Unaweza kuwapata watu wa rika zote lakini watoto wenye umri wa chini ya miaka 15 ndio wanaoathirika zaidi. Ugonjwa huu hushambulia mishipa ya fahamu hatimaye husababisha kupooza kwa misuli, hasa ya miguu, mikono au yote kwa pamoja, na pengine misuli ya kiwambo (diaphragm) na kusababisha kifo. Kila mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja ni lazima awe amekamkilisha chanjo ya kuzuia ugonjwa wa polio kwa kupata matone mara nne ili kupata kinga kamili. Yaani chanjo ya kwanza mara tu azaliwapo, ya pili akiwa na wiki sita, ya tatu katika wiki ya 10 na ya nne akiwa na wiki 14.
 
Pepopunda
ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa “clostridium tetani”. Vimelea hivi huingia mwilini kupitia kwenye kidonda au jeraha. Ugonjwa huu huwapata watu wa rika zote. Kwa watoto wachanga toka kuzaliwa hadi kufikia umri wa siku 28, vimelea huingia mwilini kupitia kwenye kitovu kilichokatwa kwa kutumia kifaa chenye maambukizi, kama vile wembe, mabua na usinge au kuwekwa vitu vichafu kama vile kinyesi cha ng’ombe, vumbi la kizingitini na kadhalika.
[emoji22][emoji22][emoji22]Je, unajua kwamba ugonjwa wa pepopunda hauna tiba?
Ugonjwa huu unaua takribani watoto wote wanaoupata! Ni muhimu wanawake wote wenye umri wa kuzaa kati ya miaka 15 hadi 49 wapate chanjo kamili dhidi ya ugonjwa wa pepopunda, ili kumkinga mtoto atakayezaliwa. Zingatia usafi wakati wa kuzalisha, kukata na kutunza kitovu. Kuzuia maambukizi, kitovu cha mtoto kisiwekwe kitu chochote. Wazazi/walezi watunze kadi ya chanjo ya pepopunda kwa ajili ya kumbukumbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…