Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SHINIKIZO LA DAMU (PRESHA), MATATIZO YA UZAZI, KUONDOA KITAMBI:

Naye Dk. Zawadi Abdallah wa kituo cha dawa asili cha Zawadi Herbarist cha Tabata jijini hapa, anasema ufuta hutibu matatizo ya moyo na shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) ambapo mara baada ya kula ufuta hushuka na kuwa la wastani kwa muda mfupi ikiwa matumizi yake yatazingatiwa.
 
Ufuta huweza kuimarisha moyo na kuulinda usishambuliwe na magonjwa ikiwa ni pamoja na kushusha `presha’ ya juu kutokana na virutubisho hivyo,”alisema.
Pia kiwango protini cha kiasi cha gramu 4.7 kilichomo ni lishe muhimu kwa watoto wadogo kutokana na virutubisho na misombo hiyo kusaidia kuimarisha afya ya mtoto, kukua haraka na kumkinga dhidi ya magonjwa.
 
Zaidi anasema, unapoliwa kwa wingi hufanya kazi muhimu ya kuzibua mirija ya uzazi kwa jinsia zote, kuimarisha na kuboresha mbegu za kiume, hali ambazo kwanzo huruhusu mwanamke kushika mimba au mwanamume kuwa na uwezo kutungisha mimba.
 
Anafafanua zaidi: Mafuta ya ufuta ni mazuri kwa afya ya mwili kwa kuwa yametokanana na mbegu za ufuta, hivyo yakitumiwa kwa kuzingatia ushauri, huondoa mafuta mabaya (lehemu) mwilini na kubaki na mafuta yanayohitajika hivyo kuondokana na tatizo la kitambi na madhara mengine ya moyo.
 
MATATIZO YA FIGO, KIBOFU:

Nao utafiti wa Dk. Kurian ambao matokeo yake aliyachapisha katika kitabu chake kinachojulikana kama Healing Wonders, anasema kwa ujumla zao la ufuta ni tiba muhimu katika tiba ya figo ikiwamo kuondoa mawe kwenye figo na matatizo ya kibofu.
 
Pia una uwezo wa kutibu kipindupindu na kuzuia kuhara, kuweka sawa homoni zinazosababisha mzunguko wa hedhi kwa mwanamke kwenda sawa, alisema na kuendelea…
Huongeza nguvu kwenye mifupa na kuimarisha misuli mwilini kutokana na kirutubisho cha Kalishiamu kilichomo. Unazuia na kutibu maumivu ya tumbo ya ghafla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…