Hata hivyo, tafiti mbalimbali za ndani na nje ya nchi, zinaonesha kuwa ulaji wake ni kinga na tiba ya magonjwa katika mwili wa binadamu.
Baadhi ya magonjwa hayo ni kisukari, shambulio la moyo, kuimarisha mmengenyo wa chakula, huondoa lehemu, huboresha ngozi, huondoa na kukinga saratani na kuongeza damu.
Dk. Raphael Nyampiga ni mtaalamu wa tiba lishe katika kituo cha huduma hiyo kilichopo Pugu nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, anataja faida zingine kuwa ni kuzuia maradhi ya kinywa.
Pia huimarisha mfumo wa upumuaji, lishe kwa watoto wadogo na kuimarisha afya ya nywele na hivyo kuzuia tatizo la nywele kunyonyoka na kuota nywele kwa wale wenye uhaba au kutoota nywele.
Hiyo ni kutokana na aina mbalimbali za virutubisho vilivyomo katika mbegu za ufuta kama vile, protini, mafuta, madini kadhaa kama ya kopa, kalishiamu (calcium), chuma, zinki, fosforasi, manganizi, magineziamu na thiamine.
Huzuia na kutibu ugonjwa huo kutokana na mbegu zake kuwa na madini ya magneziamu ambayo yakiwa mwilini huzuia visababishi vya sukari kama vile tatizo la insulini na kongosho kutofanya kazi ipasavyo.
Pia mafuta ya ufuta huimarisha kuta za plasma na hatimaye kuwa na uwezo zaidi wa kuweka sawa kiwango cha sukari kwenye damu, alisema.
Dk. Nyampiga anaongeza kwa kusema kuwa, mtu mwenye matatizo ya kukosa choo au choo kigumu, anapaswa kula kwa wingi ufuta kutokana na virutubisho hivyo kurahisisha mmeng’enyo wa chakula na kufanya hali hizo kutoweka na kuondokana na tatizo la ugonjwa wa bawasiri.
Kuhusu ugonjwa wa Saratani, anaongeza kwa kusema kuwa mbegu za ufuta zina misombo (compounds) kama vile asidi aina ya phytic madini ya maginesiamu na phytosterols ambayo kwa pamoja huukinga mwili na kundoa sumusumu zinasababisha saratani.
Ufuta pia ni tiba ya matatizo yanayokabili kinywa. Kwa miaka mingi sasa watu wa jamii la kabila la Ayurveda huko barani Asia, wamekuwa wakitumia mafuta ya ufuta kama tiba na kinga ya matatizo ya kinywa ikijumuisha meno, fizi na kingo za mdomo au kinywa,”alisema Dk. Nyampiga.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.