Katika bakuli la ukubwa wa kati, changanya unga wa ngano, “baking powder”, “baking soda”, na chumvi. Changanya maziwa na vanilla katika kikombe cha kupimia. Kwa kutumia miksa katika speed ya chini, changanya viungo vikavu kwenye mchanganyiko wa mayai, ukibadilishana na maziwa (mayai...maziwa...mayai...) ukianzia na kumalizia na viungo vikavu. Changanya hadi vichanganyike sawa sawa. Kwa kutumia kijiko, weka siagi kwenye kikaango (au vikaango, kutegemea kiasi ulichonacho).