NDEGE WA AJABU. Baada ya watoto kumtoboa macho mwenzao wakakimbia, hasa baada ya mwenzao huyo kuangua kilio kutokana na maumivu makali aliyopata baada ya kutobolewa macho yake. Watoto wale kila mmoja ameenda kwao na kunyamaza kimya.wakiogopa kucharazwa bakora na wazazi kutokana na kitendo walichomfanyia mwenzao. Wazazi wa kijana aliyetobolewa macho walimtafuta kijana bila mafanikio, jitihada za kumpata usiku ule zilishindikana, hata watoto wale walipoulizwa waliasema hawajui mahali alipo kwakuwa waliachana naye muda mrefu. Kijana aliyetobolewa macho alihangaika kurudi nyumbani lakini alipotea na kufika chini ya mti mmoja mkubwa. Kwakuwa usiku ulikuwa unaingia bwamdogo akaona bora ajihifadhi mahali hapo mpaka asubuhi ili atafute njia ya kurudi kwao.