Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

T.I.-SALUTE.jpg
 
Nice song
Napenda sana hii ngoma mkuu
Ndani ya Album yake ya kwanza yenye jina MISS THANG.

MONICA ndio anatoka hapo.

Album yake hii ina Vibao ambavyo navikubali sana ikiwemo,

Before you walk out of my life.

Why I love you so much
.

Don't take it personal.

Ikiwemo na Miss thang yenyewe ambayo ndio inayobeba jina la Album
 
KAMATI TENDAJI,
CHAMA CHA SOKA (UK)

*YAH: NIA YETU YA KUTOONEKANA UWANJANI 5 NOV, 2017*


Rejea kichwa cha habari hapo juu.

Sisi kama mashabiki wa Arsenal, hadi sasa tumekumbwa na *Taharuki* kubwa kufuatia *mambo yasiyoeleweka* ambayo yamekua yakifanywa na hii timu ya *Man City*.

Kuanzia msimu huu uanze hatujui hasa hawa Man City wana Mpango gani.

Ilianza kama masihara hivi, *Liverpool wakala 5*

Wakaja *Feyenoord wakala 4*

Wakaja *Watford wakala 6*

Wakaja *Crystal palace wakala 5*

Juzi hawa wenzetu ambao tulikua tunawategemea *Stock city wakala 7*[emoji26]

Sasa sisi tunaona namba inazidi kuongezeka tuu na hatujui nia hasa ya hawa jamaa ni nini.

Sasa *sisi ni watu wazima na tunafamilia zetu nyumbani na wake zetu wanatuheshimu*,...

Tumekaa tukatafakari tumeona bora tuwaandikie barua nyinyi chama cha soka cha uingereza, kwamba tunaomba tuu muwape hao Man City hizo point 3, timu yetu haitakuja uwanjani hiyo tarehe 5 November.

*Kwani Point 3 kitu gani bwana? Shida ni yale Magoli* Wapeni tuu hizo point 3 sisi tumekubali.


Kwa namna hali ilivyo, namba ya Juzi ilikua goli 7! Sasa hatujui wana mpango gani na sisi maana *hadi sasa hawaeleweki*

Au wanataka kutupiga *Course work*, maana wenzetu ndo hao washapigwa *wiki*

Mwisho tunawaomba mufikirie iwekwe sheria ya *KNOCK ~ OUT* kama kwenye ngumi.Yani pale kwenye ngumi ukiona ngumi zimekuzingua, ukinyoosha mikono juu, basi pale pale *Game over!*,na ushindi anapewa mpinzani.

Sasa na huku kwenye mpira muweke hiyo, Timu ikishaona imezidiwa *wakae chini timu nzima pale pale uwanjani*, na game iishie pale pale. Sio kuendelea kushindiliwa magoli.

Tunaoumia ni sisi Mashabiki huku mtaani.

Ni sisi Mashabiki wa Arsenal wa Tanzania
Ahsanteni
 
Back
Top Bottom