Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5f6a43707ea1ea4693adfc7eb9768210.jpg
 
Anaemia ni jina jumla linalotumiwa kubainisha aina mbalimbali za upungufu wa damu mwilini.
Vipi Inatokea?
Upungufu huo wa damu hutokea iwapo ukolezi au mkusanyiko wa pamoja wa chembe nyekundu za damu (haemoglobin) vinapopungua kupita kiwango cha kawaida. Kwa ufupi Anaemia husababishwa na mambo makuu matatu yafuatayo:
 
. kuharibiwa kwa chembe nyekundu za damu kunakosababishwa na magonjwa ya kurithi (hereditary), magonjwa kama vile kansa au athari mbaya zinazotokana na utumiaji wa baadhi ya dawa.
Hadi hapa mpenzi msikilizaji umetambua sababu za ugonjwa wa Anaemia na bila shaka ungependa kujua dalili za ugonjwa huo.
 
Dalili za Anaemia au upungufu wa damu ni zipi (isisomwe)
-Mtu mwenye tatizo la upungufu wa damu mara nyingi huwa amepauka mwili na huwa na dalili zifuatazo:
1. hujisikia kuchoka .2. dhaifu na huwa na mwendo kasi wa damu (yaani high pulse rate). 3. huhisi kiu, 4. kizunguzungu wakati akisimama 5. Huhema na kuwa na mpapatiko wa moyo wakati akitumia nguvu.
Kuna aina mbalimbali za Upungufu wa Damu au Anaeamia. Kwanza ni:
 
Iron defiency anaemia (Huu ni upungufu wa damu anaopata mtu wakati anapopoteza kiwango fulani cha madini ya chuma mwilini. Itafahamika kuwa mwili wa wanadamu unahitaji madini ya chuma ili kuweza kuzalisha chembe nyekundu za damu. Na vile vile itakumbukwa kuwa, iwapo mtu atapoteza kiasi fulani cha damu, madini ya chuma nayo hupungua mwilini na hivyo kusababisha upungufu wa madini hayo kwa muda. Ulaji wa madini ya chuma katika mlo wa kawaida wa mtu hauwezi kufidia kiwango cha madini kilichopotea, kwa hiyo akiba ndogo iliyobakia mwilini ya chuma hutumika mara moja
 
Kwa hakika upungufu wa damu unaosababishwa na ukosefu wa madini ya chuma au Iron deficiency anaemia, huathiri watu wengi duniani.
Swali linalojitokeza hapa ni kuwa je, upungufu huu wa damu huwapata akina nani zaidi?.
 
Back
Top Bottom