Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1508863386865.jpg
 
Waswahili wanao usemi maarufu kuwa, raha ya nyumba ni choo.Kwa hakika, hawakukosea kwani chakula chochote kinapoliwa lazima kitumike mwilini na mabaki yake kutolewa kwa njia ya haja kubwa.
 
Hata hivyo, binadamu wa jinsi zote, umri au rika baadhi yao wanakabiliwa na tatizo la kukosa choo, ambalo linawasumbua kweli. Tatizo hilo ambalo huzaa au kuambatana na tatizo jingine la kupata choo kigumu linatesa.
 
Kwa kawaida, mtu anapopata tatizo hili hutumia muda wake mwingi chooni akijaribu kusukuma haja kubwa wakati mwingine bila mafanikio.

Ni dakika chache zinazohitajika kumaliza haja inapotoka kwa urahisi, lakini kwa wenye tatizo hilo, dakika hizo hazitoshi kwao kumaliza haja.

Ugumu wa kuitoa haja hiyo huwasababishia maumivu makali na pengine kuzalisha maradhi mengine.
 
Kwa mtu anayeishi kwenye nyumba ya kupanga na yenye wapangaji wengi wanaotegemea chumba kimoja cha choo zikiwamo zile za mijini, mmoja wao anapokuwa na tatizo hili la kupata choo kigumu inaweza kuwa kero kwa wenzake.
 
Kwa ufupi, mtu anapoingia chooni kujisaidia, wenzake hukaa nje wakisubiri kwa muda zamu zao za kuingia…hakika huwa ni mateso kwake na kero kwa wapangaji wenzake.
 
Tatizo la kukosa choo (constipation)

Kukosa choo kwa siku moja kitaalamu, siyo tatizo, isipokuwa mtu anaweza kutajwa kuwa na tatizo hilo iwapo atakosa choo kwa angalau zaidi ya saa 72, yaani siku tatu.
 
Akizungumzia tatizo hili, Mtaalamu wa Viungo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) , Dk Raymond Mwonekano anasema kwa kawaida kila mtu anatakiwa apate choo angalau mara tatu kwa wiki. “Kama mtu atakosa choo kwa siku tatu mfululizo, atahesabika kuwa na tatizo, lakini lazima awe amekula chakula kwa siku zote hizo.

Mtu ambaye hajala hawezi kuhesabika kuwa na ugonjwa huo bali atakuwa na tatizo jingine,” anasema.
 
Anaongeza kuwa tatizo hilo linatokana na haja kubwa kwenda taratibu na hivyo kuchelewa kutoka kwa wakati mwafaka.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo la haja kubwa zikiwemo za kutojizoeza kwenda haja kubwa mara kwa mara, kula vyakula vilivyokobolewa, matumizi mabaya ya dawa, mabadiliko ya homoni na magonjwa mengine ya mwili.
 
Matatizo ya kisaikolojia

Naye Dk Michael Mngwatu kutoka Hospitali ya Mico iliyoko Tabata jijini Dar es Sakaam anasema, wakati mwingine mtu anaamua kutojisaidia kwa sababu mbalimbali kwa makusudi, jambo linaloweza kumsababishia tatizo hili la kukosa choo kama hali hii itajirudia mara kwa mara. “Kuna wakati mtu anaamua tu siendi kujisaidia saa hizi, nitaenda baadaye. Mwingine huamua kujibana kwa kuogopa kutumia choo fulani hasa vile vya umma,” anasema Dk Mngwatu.
 
Anaongeza kuwa hali hii ikijirudia mara kwa mara inatengeneza tatizo la kisaikolojia la kushindwa kujisaidia kwa wakati.

Magonjwa mengine ya kukosa choo

Kukosa choo linaweza kuwa tatizo, lakini kama halitapatiwa ufumbuzi linaweza kuzaa matatizo mengine mwilini.

Dalili za kuwa na tatizo la kukosa choo kwa mujibu wa Dk Mngwatu ni kwamba mgonjwa anaweza kupata maumivu ya tumbo ambayo hutokana na tumbo kujaa gesi. “Mtu mwenye tatizo la kukosa choo mara nyingi tumbo lake huvimba na kujaa gesi muda wote, hali hii inatokana na kuwa na uchafu tumboni,” anasema.
 
Back
Top Bottom