Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anaongeza kuwa kukosa choo kunaweza pia kusababisha maambukizi katika utumbo ambayo yanaweza pia kusababisha magonjwa mengine ukiwamo wa kuoza kwa sehemu ya utumbo.

“Kinyesi kinapokwama mahali, eneo lile linaweza kukandamizwa na kukosa damu, hivyo linaweza kuoza,” anasema mtaalamu huyo.
 
Anaongeza kuwa kukosa choo kunaweza pia kusababisha maambukizi katika utumbo ambayo yanaweza pia kusababisha magonjwa mengine ukiwamo wa kuoza kwa sehemu ya utumbo.

“Kinyesi kinapokwama mahali, eneo lile linaweza kukandamizwa na kukosa damu, hivyo linaweza kuoza,” anasema mtaalamu huyo.
 
Anasema ugonjwa mwingine unaoweza kuupata kwa kukosa choo ni uvimbe katika njia ya haja kubwa (Bawasiri) ambao nao husababishwa na kuchubuka mara kwa mara wakati wa kujisaidia.

“Ngozi ya njia ya haja kubwa inapopata michubuko mara kwa mara, hupasuka na kusababisha vivimbe vidogo ambavyo huweza kukua kadri hali hiyo inayoendelea,” anasema.
 
Screenshot_2017-10-24-19-42-21.png
 
Dalili za kukosa choo

Dk Mngwatu anasema mgonjwa anayekosa choo anaweza kujua tatizo hilo limeshika hatamu iwapo tu dalili nyingine mbali na kukosa choo zitaanza kujionyesha.

Anazitaja dalili nyingine kuwa ni pamoja na: Kupata homa kali, kutetemeka kwa baridi, kutapika na kupata vidonda nje ya njia ya haja kubwa.
 
Anaongeza kuwa kwa kawaida tatizo hili huwapa watu mbalimbali duniani kote, lakini hutofautiana ukubwa wake kutokana na staili ya maisha, kwani wengine huwa wepesi kuligundua na kulitafutia ufumbuzi. “Karibu kila mtu duniani katika hatua fulani ya maisha hupata tatizo hili, kutokana na sababu za vyanzo vyake watu hupitiwa au kwa makusudi huacha kufuata kanuni na kujikuta wamepata tatizo hili,” anasema mtaalam huyo.
 
Akitolea mfano anasema wakati wa sherehe au mikusanyiko ya watu huwa ni vigumu kuchagua aina ya vyakula na wakati mwingine matunda na maji ya kutosha hukosekana hivyo kuwafanya watu wale vyakula vigumu ambavyo vinaweza kuchochea tatizo hili.

Kinga na matibabu yake

Dk Mwonekano anasema kila mtu anao uwezo wa kujikinga na tatizo hili kwa kufuata kanuni za ulaji chakula bora.
 
Kwa asilimia kubwa, tatizo hili linasababisha na namna unavyokula au kuishi, kama ukifuata zile kanuni za ulaji chakula bora tatizo hili halitakupata,” anasema Dk Mwonekano.

Anafafanua kuwa njia sahihi ya kujikinga na ugonjwa huo ni kula nafaka zisizokobolewa, matunda, mboga mboga na kunywa maji kwa wingi.

Kuhusu matibabu halisi anasema iwapo tatizo litagundulika mapema ni rahisi kulikabili kwa kubadilisha mfumo wa ulaji akitolea mfano mtu anapokosa choo na kuamua kula mapapai kwa wingi .
 
Kama umekosa choo kwa muda mrefu, zipo njia ambazo unaweza kuzitumia hapo nyumbani, tumeshafanya hivi mara nyingi katika maisha yetu na imetusaidia,” anasema.

Anaongeza kuwa kama mgonjwa akishindwa kutumia tiba mbadala ambazo ni pamoja na kula matunda, mboga na kunywa maji mengi, anaweza kutibiwa kwa kupewa dawa mbalimbali ambazo zinaweza kumsaidia ili apate choo.

Hata hivyo, hilo linaposhindikana kwa njia zote hizo, mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuondoa kinyesi kile kilichoganda na kumwanzishia matibabu ya kumfanya aweze anajisaidia kwa urahisi.
 
Tatizo kwa watoto

Kama ilivyo kwa watu wazima, watoto tangu kuzaliwa wanategemewa kupata choo, lakini nao pia wanaweza kukumbwa na tatizo hili. Kila linapowapata tatizo hili, wengi wa watoto hao hubadilika tabia au hata mazoea na wakati mwingine huanza hata kulia, kulalamika kuwa wanahisi maumivu ya tumbo.

Wengine kati yao huanza kujibana maumbile yao, kujificha katika sehemu za siri nyumbani kwao, wakiogopa kusema hata kwa wazazi au walezi wao.
 
Kukosa choo kwa wajawazito

Tatizo hili ni mojawapo ya shida kubwa zinazowapata wajawazito wengi.

Watalaamu wanakadiria kuwa hadi asilimia 50 ya wajawazito hupata tatizo hilo kwa wakati mmoja.

Hata hivyo, wanashauri kwamba linapotokea na kuwa vigumu kujisaidia, tatizo hili linaweza kuzuiwa kirahisi kwa kubadili aina ya ulaji.
 
Wanawake wajawazito wanashauri kufanya mambo mengi yakiwamo mazoezi ili kujiepusha na tatizo hilo.

Kukosa choo kwao kutokana na kukua kwa tumbo na kiumbe kilichomo mwilini na kuongeza shinikizo kwenye viungo vya mwili wake na kubadili homoni kiasi cha kuathiri mfumo wa umeng’enyaji chakula.
 
Back
Top Bottom