Kama umekosa choo kwa muda mrefu, zipo njia ambazo unaweza kuzitumia hapo nyumbani, tumeshafanya hivi mara nyingi katika maisha yetu na imetusaidia,” anasema.
Anaongeza kuwa kama mgonjwa akishindwa kutumia tiba mbadala ambazo ni pamoja na kula matunda, mboga na kunywa maji mengi, anaweza kutibiwa kwa kupewa dawa mbalimbali ambazo zinaweza kumsaidia ili apate choo.
Hata hivyo, hilo linaposhindikana kwa njia zote hizo, mgonjwa anaweza kufanyiwa upasuaji mdogo ili kuondoa kinyesi kile kilichoganda na kumwanzishia matibabu ya kumfanya aweze anajisaidia kwa urahisi.