Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2017-10-25-18-39-35.png
 
Facebook yahusika katika kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja

Watu wengi hasa nchini Nigeria wameweza kukuza vipato vyao vya kila siku kwa kutumia mtandao wa Facebook kutangaza bidhaa zao wakitumia simu janja kuingia katika mtandao huo na kutangaza biashara zao na kuweza kukuza soko la bidhaa zao ndani na je ya Afrika kwa kutumia Facebook.
 
Google play ndio soko linaloongoza kwa App za bure ukiachana na masoko mengine kama lile la AppStore linalomilikiwa na Apple Inc.

Soko la Google Play kama jina lake lilivyo linamilikiwa na kampuni ya Google, sasa ili kujua mbinu tofauti kuhusiana na soko hili endelea kusoma zaidi
 
FUATILIA SIMU ILIYO POTEA AU KUIBIWA

Ndio unaweza kufuatilia simu yako iliyopotea au kuibiwa lakini simu yako ya Android inabidi iwe na vitu muhimu vitatu ambavyo ni

Kifaa chako kiwe kimeunganishwa na akaunti yako ya google
Kifaa chako lazima kiwe na uweza wa kuingia katika mtanadao (ineternet)
Lazima kifaa chako kiwe kimewasha sehemu ya ‘Location Settings’
 
FUTA DATA ZAKO ZOTE KWA KUTUMIA GOOGLE PLAY

Hii ni moja kati ya zile mbinu nzuri tuu unazoweza fanya ukiwa na kifaa chako cha Android. Kwa kutumia njia hii unaweza uka RESET skifaa/simu yako ya android lakini kifaa hiko lazima kiwe na mambo mawili ya muhimu

Hakikisha kina uweza wa kimtandao (internet)
Hakikisha kifaa chako kimeunganishwa na akaunti ya google
 
Kama una uhakika kifaa chako kimekidhi mambo yote hayo basi nenda katika ‘Android Device Manger‘ kisha futa kila kitu katika simu yako iliyoibiwa au kupotea. Hii itahakikisha usalama wa vitu vyako (mfano Picha, nyaraka, video na mafaili mengine ya muhimu) ndani ya kifaa.
 
RUDISHIWA KIASI ULICHOTUMIA NUNUA APP USIYOIPENDA

Hivi umenunua App ambayo baadae haifanyi kazi kama ulivyodhani au hukuipenda na akajuta kupoteza hela yako bure?. Sasa unafanyaje?

Google rudisha kiasi ulichotumia kwa App ambazo hazifanyi kazi kama ulivyotegemea lakini kwa zoezi hili kukamilika kuna vigezo na masharti ambayo inabidi yazingatiwe.. zoezi hili litafanyika mara moja tuu kwa kila App hivyo usije kujisumbua kuomba kurudishiwa kiasu chako zaidi ya mara moja. Kitu kingine ni kwamba unaweza omba kurudishia kiasi chako baada ya masaa mawili kupita tangia ulivyo nunua App hiyo.
 
Ili kurudishiwa kiasi chako, fungua Google play store na itafute hiyo App ya kulipia uliyoishusha. Ikishatokea ataona sehemu imeandikwa ‘REFUND’ bofya juu yake na Google ita rudisha kiasi hicho ndani ya masaa 48. Kitu kingine kizuri kuhusu hii ni kwamba hakuna sera ya maswali kwa hiyo unaweza omba kurudishiwa kiasi chako. Hii inamaanisha huwezi kuulizwa maswali mia ili kurudishiwa kiasi chako.
 
Back
Top Bottom