Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MAMBO KUMI USIYOYAFAHAMU KUHUSU UGONJWA WA KICHAA CHA MBWA.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO), yafuatayo ni mambo kumi yahusianayo na ugonjwa wa kichaa cha mbwa (Rabies).
 
Ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na huwa ni hatari hatua zisipochukuliwa haraka na dalili kujitokeza na kusababisha kifo. Ugonjwa huu huwaathiri wanyama wa kufugwa hata wale wa mwituni, na binadamu hupata ugonjwa endapo atagusana na mate ya mnyama mwenye ugonjwa kupitia kung’atwa meno au mkwaruzo kutoka kwa mnyama mwenye ugonjwa. Dalili za mwanzo za ugonjwa ni homa, kuhisi kuchomachoma katika eneo lililong’atwa au kukwaruzwa. Kusafisha eneo lililong’atwa au kukwaruzwa ndani ya muda mfupi pamoja na kupata chanjo ya kukinga ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni njia thabiti ya kuzuia kupata ugonjwa huu.
 
Ugonjwa wa kichaa cha mbwa upo katika mabara yote isipokuwa bara la Antaktika. Maelfu ya watu hupoteza maisha kila mwaka na zaidi ya 95% ya vifo huwa vinatokea barani Afrika na Asia.Ugonjwa huu ni ugonjwa uliopuuziwa na huwaathiri watu masikini hasa katika maeneo ya vijijini ambapo hakuna hatua mahususi ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
 
Mbali na mbwa au popo, pia wanyama wengine waweza kueneza ugonjwa huu. Ingawa mbwa ni mnyama anayeeneza ugonjwa huu zaidi barani Afrika, kwa upande mwingine popo ndiye mnyama anayeeneza ugonjwa huu kwa binadamu zaidi barani Amerika. Kwa hiyo vifo kwa binadamu hufuatia maambukizi ya ugonjwa kutoka kwa wanyama kama mbwa mwitu, mbweha, nguchiro na vinyegere na wanyama wengine walao nyama.
 
Asilimia 40 ya wanaong’atwa na mbwa wazururao ni watoto wa chini ya miaka 15. Watoto kutokana na asili yao ya kuwa wachangamfu na kupenda michezo, hujikuta wakiwakaribia mbwa wakijaribu kucheza nao hata wakati mwingine kuwachokoza pasipo kujua hatari ya ugonjwa uenezwao na wanyama hao. Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa, watoto wengi wanapong’atwa au kukwaruzwa na mbwa, huwaficha wazazi wao kwa hofu ya kuadhibiwa, na dalili za ugonjwa zinapotokea huwa ni vigumu kutibu au kuzuia na watoto hupoteza maisha.
 
Msichana yeyote anayemsaliti mpenzi wake, moto umuwakie, meno ya mbele yatoke, nywele kichwani zitoke na pia apinde miguu..

Kwa mvulana anayemsaliti mpenzi wake, eee Baba tusamehe sisi, tufundishe tuyafate matendo yako, kwani hatujui tulitendalo...


[emoji85][emoji85][emoji85][emoji85][emoji85]
 
Matibabu ya mapema baada ya kung’atwa na mbwa ni muhimu ili kuokoa maisha. Ni vyema jeraha kusafishwa haraka kwa kutumi maji safi na sabuni, ikifuatiwa na chanjo ya kuzuia ugonjwa. Baada ya hapo mwathirika ataendelea na kozi kadhaaa za chanjo. Kila mwaka zaidi ya watu milioni 15 hupatiwa chanjo ya kichaa cha mbwa. Chanjo hizi huzuia kuenea kwa ugonjwa huu, na inakadiriwa kuwa, chanjo hizi huzuia mamia ya maelfu ya vifo kutokana na ugonjwa huu kila mwaka.
 
Chanjo kwa mbwa husaidia kuzuia maambukizi kuenea. Uchanjaji wa angalau 70% ya mbwa, ukijumuisha mbwa wazururao, husaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa kwa binadamu na ni njia mahsusi ya kutokomeza ugonjwa.Mfano, kampeni ya uchanjaji wa mbwa huko Bangladesh, iliwezesha kupungua kwa zaidi ya 50% ya vifo kwa binadamu kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa kati ya mwaka 2010 na 2013. Hii imedhihirika pia nchini Tanzania, Ufilipino na katika jimbo la Kwazulu Natal, ambapo kampeni za chanjo zimefanikiwa kupunguza vifo kwa asilimia kubwa.
 
Chanjo kwa mbwa husaidia kuzuia maambukizi kuenea. Uchanjaji wa angalau 70% ya mbwa, ukijumuisha mbwa wazururao, husaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa kwa binadamu na ni njia mahsusi ya kutokomeza ugonjwa.Mfano, kampeni ya uchanjaji wa mbwa huko Bangladesh, iliwezesha kupungua kwa zaidi ya 50% ya vifo kwa binadamu kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa kati ya mwaka 2010 na 2013. Hii imedhihirika pia nchini Tanzania, Ufilipino na katika jimbo la Kwazulu Natal, ambapo kampeni za chanjo zimefanikiwa kupunguza vifo kwa asilimia kubwa.
 
Gharama ya kuwachanja mbwa kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni nafuu ukilinganisha na gharama ya chanjo ya kuzuia ugonjwa kwa binadamu. Kwa wagonjwa wengi wanaong’atwa na mbwa mwenye ugonjwa, gharama za chanjo ya kuzuia ugonjwa, huwa ni ghali mara nyingi sana ukilinganisha na kipato cha mgonjwa kwa siku.
 
Usajili na ufuatiliaji wa wanyama wafugwao nyumbani husaidia kupambana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Hii husaidia katika mipango ya utoaji huduma kwa wanyama hao zikiwemo chanjo. Katika usajili wa mbwa, mnyama hupewa namba ya leseni ya utambulisho ambayo humuweka mnya ma katika mkakati wa kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Hii hupelekea kuzuia kusambaa kwa ugonjwa kwenda kwa binadamu.
 
Kuwaelimisha watoto ni muhimu ili kuepuka kung’atwa na mbwa au wanyama waenezao ugonjwa. Shirika la afya duniani (WHO) kama sehemu ya juhudi hizo wakishirikiana na wadau wengine kuelemisha jamii pamoja na kuongeza uelewa dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, pamoja na kuwasaidia wamiliki wa wanyama kuwahudumia wanyama wao, imesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa.
 
Ushirikiano wa sekta mbalimbali ni muhimu ili kuzuia uambukizi wa ugonjwa wa kichaa cha mbwa. Shirika la afya duniani, linashirikiana na wadau katika kilimo na mifugo ili kuwezesha katika upatikanaji wa chanjo bora na salama. WHO pia inashirikiaka na serikali mbambali katika kuimarisha huduma za maabara pamoja na kampeni za afya.
 
Kukosa usingizi kwa watu wazima na wenye umri mkubwa kwaweza kusababishwa na yafuatayo: Kwanza ni utaratibu usio mzuri wa kulala pamoja na mazingira ya kulala. Hii ni pamoja na muda usio rasmi wa kulala au muda unaobadilika badilika kila siku, unywaji wa pombe kupindukia au kunywa pombe muda mfupi kabla ya kulala, au kulala usingizi kabla haujazima runinga au redio.
 
Pili maumivu ya mwili yanayosababishwa na magonjwa mbalimbali. Maumivu huchangia sana kukosekana kwa usingizi kwa watu wenye umri mkubwa. Kwa nyongeza , sababu nyingi za kiafya kama kukojoa mara kwa mara nyakati za usiku, magonjwa ya viungo (kwa kitaalamu arthritis) , pumu, kisukari, mmomonyoko wa mifupa, kiungulia nyakati za usiku, kukoma kwa hedhi kwa kina mama na maumivu kutokana na magonjwa mengine mengi huchangia pia ukosefu wa usingizi.
 
Tatu matumizi ya dawa mbali mbali. Watu walio na umri mkubwa hutumia dawa za tiba kwa wingi ukilinganisha na wale walio na umri mdogo na mara nyingi hutumia mchanganyiko wa dawa aina nyingi. Kwa hiyo maudhi ya dawa (side effects) moja moja atumiazo mtu yanaweza kupelekea kukosekana kwa usingizi.
 
Nne ni ukosefu wa mazoezi ya mwili. Kama umezoea maisha ya kukaa sehemu moja muda mrefu bila kufanya chochote au mazoezi, unaweza kukosa usingizi nyakati za usiku au kujisikia katika hali ya kulala lala hasa nyakati za mchana. Mazoezi ya ndani au ya nje nyakati za mchana au mazoezi angalau masaa matatu kabla ya kulala huchangia mtu kupata usingizi mnono.
 
Nne ni ukosefu wa mazoezi ya mwili. Kama umezoea maisha ya kukaa sehemu moja muda mrefu bila kufanya chochote au mazoezi, unaweza kukosa usingizi nyakati za usiku au kujisikia katika hali ya kulala lala hasa nyakati za mchana. Mazoezi ya ndani au ya nje nyakati za mchana au mazoezi angalau masaa matatu kabla ya kulala huchangia mtu kupata usingizi mnono.
 
Back
Top Bottom