Lengo la ulaji wa chakula bora kwa afya bora ni kujenga tabia ya kula aina ya lishe bora ambayo utaendelea kula kwa maisha yako yote, siyo tu kwa wiki chache au miezi michache mpaka pale utakapokuwa umefikia uzito ulio sawa kwa afya. Kwa hiyo jaribu kufikiri kiasi ambacho kinakutosha ili mwili uendelee kuwa na afya njema katika uzito unaokubalika wa mwili na ulaji uwe katika msingi wa mlo kamili( balanced diet).Mbali na kuwa tunapenda vyakula vyenye ladha fulani, tunahitaji pia kuzingatia mlo kamili wenye makundi ya chakula kama wanga, protini, mafuta, fiba(zapatikana katika mboga mboga,nafaka na matunda), vitamini, madini na maji, vyote hivyo kwa ajili ya kuiweka miili na akili zetu katika hali ya afya bora.