Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bab_usBnhuY.jpg
 
Aaa wapi?

[emoji117][emoji117][emoji117]Asanteni nyote kwa utani wa leo. Stress zote kwisha. Kama kwa namna moja au nyingine kuna mtu kakwazika, tusameheane wapendwa. Upendo wetu na furaha hii vidumu daima !!!
Ulikuwa na stress?pole
Hii ndio raha ya uzi huu na hapo alikosekana kivuruge andjul tu
 
Katika magonjwa ambayo huwasumbua watoto mara kwa mara ni ugonjwa wa kuhara, lakini habari njema ni kuwa ugonjwa huu humalizika ndani ya siku chache mtoto anapohudumiwa vyema. Lakini pamoja na hayo ni vyema kujua jinsi ya kumsaidia mtoto anayekabiliana na ugonjwa huu na jinsi ya kuwakinga wale wasio na ugonjwa.
 
Ni nini kinachosababisha ugonjwa wa kuhara?
Kuhara ni ugonjwa ambao husababishwa kwa kiasi kikubwa na aina ya virusi, lakini pia yaweza kua bacteria au vimelea vinginevyo vya magonjwa. Mtoto(mgonjwa) hupata choo mara nyingi ambacho ni majimaji.
 
Aina ya vijimelea vinavyosababisha kuhara kwa watoto hutegemea eneo la kijiografia kulingana na viwango vya usafi wa mazingira, hali ya kiuchumi na usafi wa mwili. Kwa mfano nchi zinazoendelea ambapo hali ya usafi wa mazingira ni duni na maeneo ambayo kinyesi cha binadamu hutumika kama mbolea, hukabiliana na milipuko ya magonjwa ya kuhara mara kwa mara kwa sababu taka hizi zitokanazo na binadamu ni rahisi kuingia katika vyakula na maji ya kunywa.
 
Kwa ujumla, vimelea vinavyosababisha kuhara ni rahisi kuambukiza kutoka mtu mmoja hadi mwingine au mtu kupata ugonjwa kwa kujigusa na mazingira yaliyo na vimelea vya ugonjwa huu. Maambukizi yanayosababisha ugonjwa wa kuhara yanaweza kusambazwa kupitia: Mikono michafu iliyoshika sehemu zenye vimelea vya ugonjwa, maji machafu au chakula kilichoingia vimelea vya ugonjwa, wanyama wa kufugwa nyumbani, kujigusa katika mazingira yaliyochafuliwa na kinyesi cha binadamu na wadudu warukao na watambaao kama inzi na mende.
 
Virusi ni sababu kuu ya ugonjwa wa kuhara kwa watoto (hujulikana wakati mwingine kama “mafua ya tumbo” ambayo yaweza pia kusababisha kutapika). Kuna aina tofauti tofauti ya virusi vinavyosabisha kuhara kwa watoto, ambavyo husambazwa majumbani, shuleni na hata watoto wanapocheza na watoto wenzao. Ingawa dalili za ugonjwa huu huwepo kwa siku chache lakini waweza kuwaathiri sana watoto wachanga ambao hawawezi kunywa maji mara kwa mara na wananapata upungufu wa maji mwilini ( kwa kitaaalamu -dehydration).
 
Uambukizi wa magonjwa ya kuhara ni kawaida kuwakumba watoto walio wengi, lakini pia kuhara kunaweza kuwa dalili ya magonjwa mengine yasiyo ya uambukizi, mfano kuhara kunaweza kuashiria mzio (allergy), tumbo la mtoto linaposhindwa kumeng’enya maziwa (kwa kitaalamu-lactose intolerance) hususani anapobadilishiwa maziwa, kutoka maziwa ya mama na kutumia maziwa ya ng’ombe. Pia kuna
magonjwa mengine ambayo huathiri tumbo (kwa kitaalamu-Inflammatory bowel disease)
 
Dalili za ugonjwa wa kuhara kwa watoto
Dalili za ugonjwa huu huanza na tumbo kunyonga na hufuatiwa na kuhara ambako hudumu kwa siku chache. Uambukizi wa virusi au bakteria wasababishao kuhara yaweza kupelekea pia mtoto kupata homa, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kutapika, kupungua uzito, na upungufu wa maji mwilini.
 
Back
Top Bottom