Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakikisha watoto wananawa mikono vyema kwa maji safi na sabuni mara kwa mara, hususani baada ya kutoka chooni au kabla ya kula. Kunawa mikono ni njia iliyo thabiti katika kuwakinga watoto na maambukizi yanayosababisha kuhara na ambayo huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Mikono michafu hubeba vimelea vya magonjwa na watoto hupenda kung’ata na kunyonya vidole, kula kwa kutumia mikono au kuingiza kiganja mdomoni.
 
Hakikisha nyama ambayo haijapikwa inawekwa kwenye jokofu pindi inapofikishwa nyumbani, au kama huna jokofu hakikisha inachemshwa pindi unapofika nyumbani kutoka buchani au sokoni. Na kila baada ya mlo, vyakula vinavyobaki vihifadhiwe vizuri katika jokofu.
o Kamwe usinywe maji ya vijito, mito, chemchem, bombani au ziwani ambayo hayakuchemshwa. Pia chukua tahadhari unaponunua chakula cha mtaani kwa sababu vyakula hivi kwa asilimia kubwa huandaliwa katika mazingira machafu ambayo huwa hayakaguliwi na bwana afya.
 
Usioshe vyombo vinavyotumiwa na wanyama katika sinki moja na vyombo ambavyo hutumiwa na familia.
o Hakikisha wanyama wafugwao nyumbani wanatengewa sehemu tofauti ya kula mbali na sehemu ya kula ya familia.
Ni wakati gani unahitajika kumpeleka mtoto hospitali?
Mpeleke mtoto mchanga hospitali haraka kama amepata ugonjwa wa kuhara, na kwa watoto wakubwa walio na dalili zifuatazo:
 
Kuhara kusikoisha baada ya siku chache.
o Mtoto amepata homa.
o Kutapika mara kwa mara na mtoto hataki kunywa maji.
o Maumivu ya tumbo.
o Mtoto anaharisha damu na choo chenye makamasi.
Pia mpeleke mtoto hospitali haraka kama ana upungufu wa maji mwilini. Dalili za upungufu wa maji mwilini ni hizi zifuatazo:
 
Kuchoka na kizunguzungu kwa watoto wakubwa.
o Kukauka mdomo au ulimi kuwa mkavu.
o Machozi kidogo au bila machozi mtoto anapolia.
o Ngozi kusinyaa na kuwa kavu.
o Kukosa kupata mkojo katika muda wa saa 10 kwa watoto wakubwa au mkojo kidogo na wa njano kwa watoto wadogo
o Pampa au nepi kavu katika muda wa saa sita na zaidi kwa watoto wachanga au mkojo kidogo wa njano.
o Utosi wa mtoto unabonyea.
o Macho yamebonyea kuingia kichwani.
 
Back
Top Bottom