Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mazoezi ya mara kwa mara au kufanya kazi zinazohusisha matumizi ya nguvu ya mwili yanasaidia mifumo mingi ya mwili kufanya kazi inavyotakiwa, mazoezi yatatuepusha na magonjwa ya moyo, kisukari, na hata magonjwa mengine hayataweza kushambulia miili yetu, na ni njia nzuri ya kupunguza uzito wa mwili uliozidi. Unapokuwa unafanya mazoezi mara mara utafaidika na mambo yafuatayo:
 
Pili mazoezi yanasaidia kutulinda na magonjwa ya moyo, kiharusi na magonjwa yanayoambatana nayo kama shinikizo la damu na ongezeko au kiwango cha juu cha lehemu katika damu. Kiwango cha juu cha lehemu katika damu kimekuwa kisababishi cha ongezeko la shinikizo la damu na hata kuwa katika hatari ya kupata kiharusi.
 
Tatu mazoezi yanatusaidia kuepukana na magonjwa ya kansa fulani kama kansa ya tumbo, kansa ya matiti, kansa ya mapafu na kansa ya kizazi. Hii ni kwa sababu mazoezi yanaboresha mifumo mbali mbali ya mwili na kuwezesha mwili kutoa taka na sumu mbali mbali mwilini, pamoja na kuimarika kwa kinga ya asili ya mwili.
 
Tafiti za wanasayansi zilizofanyika hivi karibuni zinaonyesha kuwa mazoezi yanasaidia kutokupoteza uwezo wa kuona. Matatizo mengi ya kuona hujitokeza mara nyingi kwa wazee, kwa hiyo tunaweza kuzuia hali hiyo isijitokeze kwa kufanya mazoezi.(kwa mujibu wa jarida la newscientist la marekani)
 
Mazoezi yanasaidia pia kutukinga na matatizo ya mmomonyoko wa mifupa (osteoporosis) ambayo mara nyingi hujitokeza uzeeni. Yanaimarisha afya ya akili, yanasaidia kutuepusha na magonjwa ya kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee. Pia mazoezi yanatuondolea msongo wa mawazo, woga na mtu kuwa katika afya nzuri ya akili.
 
Vitamini ni virutubisho vya lishe vipatikanavyo katika vyakula mbalimbali, na virutubisho hivi ni muhimu katika kusaidia mwili katika utendaji kazi wa mifumo mbalimbali . Kuna makundi mawili ya vitamini. Moja ni kundi la vitamini zinazochanganyika katika maji nazo ni vitamini B na vitamini C, na pili ni aina za vitamini zinazochanganyika katika mafuta nazo ni A,D,E na K.
 
Kirutubisho hiki ni muhimu kwa ukuaji na afya bora, ambapo huimarisha kinga ya mwili na husaidia afya ya macho na kuona vyema. Vitamini A hutusaidia kuepukana na upofu wa kuona usiku,pia husaidia kuona vyema nyakati za mchana. Beta carotene ni muhimu kwa sababu huondoa sumu mwilini zijulikanazo kama free radicals, na hii ni ile
 
Beta carotinoidi hupatikana katika vyakula vya asili ya mimea kama, Matunda ya njano kama machungwa,papai,embe,tipisi(pitches) na zabibu za pink. Pia vitamini hii hupatikana katika mboga kama, karoti,maboga,viazi vitamu, majani vya viazi vitamu (tembere),pilipili na spinachi. Kwa kawaida rangi ya njano ya matunda na mbogamboga iliyokoa sana inaashiria uwepo kwa wingi wa beta carotinoidi.
 
Upungufu wa vitamini A, husababisha kutokuona usiku, ukavu wa macho kwa kushindwa kutengeneza machozi, upofu,ngozi kavu, kupoteza uwezo wa kunusa na kukosa hamu ya kula. Upungufu wa vitamini hii husababisha mtu kuwa na kinga dhaifu hivyo kushambuliwa na maradhi.

Vitamini A huchanganyika vyema na mafuta, vyakula vyenye vitamini A vitafyonzwa vyema mwilini endapo vitapikwa kwa kutumia mafuta.
 
Back
Top Bottom