Sumu za dioxin na furan, mbali na kusababisha saratani, zimeonekana kusababisha pia magonjwa mengine kama pumu,athari katika figo,athari katika ini, ugumba na aleji kwa binadamu.
Sumu hizo pia zinapoingia katika mazingira(ardhi na maji) hudumu kwa muda wa miaka mingi. Pia hujikusanya katika miili ya wanyama wanywao maji na wapatao chakula kutoka katika mazingira hayo. Kwa kuwa sumu hizi huchanganyika na mafuta, huwa zinajikusanya kwa wingi katika sehemu zenye mafuta za wanyama hawa. Binadamu anapokula nyama za wanyama hawa naye huathirika.