Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sumu za dioxin na furan, mbali na kusababisha saratani, zimeonekana kusababisha pia magonjwa mengine kama pumu,athari katika figo,athari katika ini, ugumba na aleji kwa binadamu.

Sumu hizo pia zinapoingia katika mazingira(ardhi na maji) hudumu kwa muda wa miaka mingi. Pia hujikusanya katika miili ya wanyama wanywao maji na wapatao chakula kutoka katika mazingira hayo. Kwa kuwa sumu hizi huchanganyika na mafuta, huwa zinajikusanya kwa wingi katika sehemu zenye mafuta za wanyama hawa. Binadamu anapokula nyama za wanyama hawa naye huathirika.
 
Epuka matumizi ya mifuko ya plastiki,matumizi ya mifuko iliyotengenezwa kwa malighafi za asili ni suluhisho kubwa, kwa kuwa mifuko hii hudumu na huweza kutumika mara nyingi.
Kusanya vifaa vya plastiki na kuwapatia wakusanyaji, ambao huzirudisha viwandani kama malighafi za kutengeneza vifaa vingine.
 
Kamwe usipashe vyakula moto kwa kutumia vyombo vya plastiki(mfano kwa kutumia microwave).
Epuka vifaa vya plastiki vya watoto vya kusugulia fizi wakati meno yanapoota.
Usichome moto mabaki ya vifaa vya plastiki nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…